Wednesday, 24 July 2013

Rais Kiir avunja baraza la mawaziri


kiir 094f7Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amelivunja baraza lake la mawaziri pamoja na kumfuta kazi makamu wa rais Riak Machar katika mabadiliko makubwa zaidi kuwahi kutekelezwa katika historia ya miaka miwili ya taifa hilo.
Aliyekuwa waziri wa habari, Barnaba Marial Benjamin, ameiambia BBC kuwa mawaziri wote kutoka kwa Makamu wa Rais Riek Machar wameondolewa.
Duru zinasema haijabainika iwapo kuna waziri yeyote miongoni mwa wale waliofutwa kazi atarejeshwa katika baraza jipya la mawaziri litakalobuniwa. (HM)
Pia hakuna sababu iliyotolewa kuhusiana na hatua ya rais kuwafuta kazi maafisa hao , lakini wadadisi wanasema kuwa Bwana Kiir na makamu wake Machar wamekuwa na mgogoro wa mamlaka kwa miezi kadhaa sasa.
Sudan Kusini imekumbwa na matatizo chungu nzima hasa ya kiuchumi tangu kujitenga na Sudan mwaka 2011.
Uthabiti wake umetatizwa na malumbano kati yake na Sudan kuhusu mipaka na swala la mafuta.
Hivi karibuni baadhi ya maafisa wa Bwana Kiir, wamekuwa wakizungumzia kuwepo minong'ono kuhusu uongozi wake.
Ripoti zinasema kuwa Kiir anajitahidi kusalia na ushawishi katikachama cha Sudan People's Liberation Movement (SPLM), ambacho kinathibiti serikali.
Kwa upande wake bwana Machar, ambaye mwezi Aprili alipunguziwa mamlaka, alisema huenda akagombea uongozi wa chama cha SPLM dhidi ya rais Kiir, kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015. Chanzo: bbcswahili

0 comments:

Post a Comment