Saturday, 24 August 2013

MWANDISHI MPIGAPICHA WA KIKE ABAKWA NA KUNDI LA WANAUME AKIWA KAZINI...


Wapelelezi na maofisa wa polisi wakiwa eneo la tukio nyuma ya kiwanda hicho.
Mwandishi mpigapicha wa kike amebakwa wakati mwenzake wa kiume akifungwa na kupigwa kwenye kitovu cha biashara nchini India cha Mumbai, polisi walisema.

Kesi hiyo imerejesha kumbukumbu mbaya za tukio la Desemba la kubakwa na kufa kwa kijana mwanafunzi wa chuo kikuu katika mji mkuu wa India ambalo lilishitusha nchi hiyo.
Shambulio hilo lilitokea kwenye kiwanda cha nguo kilichotelekezwa huko Lower Parel, wilaya ya zamani ya viwanda ambayo sasa ni moja ya eneo linalokua kwa kasi ya majengo ya kifahari, maduka na baa.
Mwanamke huyo alikuwa akifanya kazi ya uhawilishaji akiwa na mwenzake wa kiume kupiga picha za kiwanda hicho usiku wa jana yake ndipo wanaume watano walipowakabili wawili hao.
Baada ya mwanzoni kutoa msaada wa kumsaidia mwanamke huyo kupata kibali cha kupiga picha ndani ya jengo hilo, wakageuka na kuwa wagomvi na kumtuhumu mwenzake wa kiume kwa kluhusika na uhalifu  katika eneo hilo.
Wakati alipokana kuhusika kwa namna yoyote walimfunga mikono yake kwa mkanda na kumpeleka mwanamke huyo sehemu nyingine ya jengo hilo na kumbaka kwa zamu, alisema Kamishna wa Polisi wa Mumbai, Satyapal Singh.
Mkuu huyo wa polisi alisema maofisa tayari wamemkamata mmoja wa watuhumiwa kuhusiana na shambulio hilo na amewataja na kuwatambua wengine wanne.
Mwanamke huyo, mwenye umri wa miaka 22, anaendelea vema kwenye hospitali moja ambako anapatiwa matibabu.
Shambulio hilo linakuja katikati ya kiwango cha juu cha uwepo wa matukio ya ubakaji nchini India.
Kubakwa na kifo cha mwanafunzi huyo ndani ya basi mjini New Delhi Desemba mwaka jana kumeitikisa nchi hiyo inayosumbuliwa kwa muda mrefu na udhalilishaji wa wanawake na kuibua migomo kutaka ulinzi madhubuti kwa wanawake.
Kuitikia hilo, serikali imepitisha sheria kali mpya zinazoongeza vifungo virefu gerezani kwa ubakaji na uchunguliaji sehemu za siri za binadamu, kunyemelea, mashambulizi ya tindikali na usafirishaji wa wanawake kuadhibiwa chini ya sheria za makosa ya jinai.
Kesi za wanaume hao wanne na mmoja mdogo watuhumiwa wa shambulio la Desemba zinatarajiwa kukamilika ndani ya wiki tatu zijazo.
Kesi dhidi ya mtuhumiwa huyo aliye chini ya miaka 18 imepangwa kusikilizwa Agosti 31. Mijadala ya kuhitimisha dhidi ya watuhumiwa wanne watu wazima ilianza Alhamisi.
Polisi imetoa hadharani michoro ya sura za watuhumiwa wanaosakwa kuhusiana na shambulio la juzi kulingana na maelezo yaliyotolewa na mwanamke huyo na mwenzake, na imeunda timu kadhaa kuwasaka watuhumiwa hao.
Kamishna Singh alisema eneo hilo ambako shambulio hilo lilitokea lilifungwa na wanaume hao wanawezekana kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwenye eneo hilo.
Shambulio hilo lilijadiliwa kwenye Bunge la India, ambako Waziri mdogo wa Mambo ya Ndani R.P.N. Singh aliwaeleza watungasheria hao kwamba serikali imelitaka Jimbo la Maharashtra, ambalo mji mkuu wake ni Mumbai, kutoa maelezo ya shambulio hilo.
Kulinganisha na Delhi, Mumbai kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kama sehemu salama kwa wanawake kusafiri peke yao, hata wakati wa usiku.
"(Mumbai) ina sifa hiyo ya ulinzi ... lakini vitu hivi vinatufanya tuhisi pengine hatuko salama kihivyo," alisema Bi A.L. Sharada, mkurugenzi wa Population First, Shirika lisilo la Kiserikali ambalo linashughulikia masuala ya haki za wanawake.
"Wanawake wanawakiwa waweze kutembea huru na kufanya kazi. Kwanini wahofie kufanyiwa mambo mabaya wakati wote?" aliongeza Bi Sharada.
Kamishna Singh alisema serikali kuu imependekeza kwamba adhabu hizo 'kali kabisa' kutolewa kwa yeyote anayepatikana na hatia katika kesi hizo.

0 comments:

Post a Comment