Kwa mujibu wa msichana huyo anadai kwamba baba yake ambaye alikuwa anakaa nchini Hispania aliporejea Ghana Desemba mwaka jana ndipo alipo anza kumtendea unyama huo.
"Katika umri wa miaka 16, nilikuwa sijawahi kulala na mwanaume yeyote yule, lakini baba yangu aliporudi kutoka Hispania Desemba mwaka jana ndipo ilianza ku s * x na mimi," alisema msichana huyo.
Msichana huyo alisema kuwa wazazi wake waliachana na tangu kuachana kwa wazazi wake baba yake ndio aliokuwa akimpa mahitaji yote na kwamba baba yake alimtishia kusitisha huduma hizo kama angemwambia mtu yeyote kuhusu kitendo hicho alicho kuwa akimfanyia.
"kulikuwa hakuna mtu mwingine wa kunilipia ada ya shule zaidi ya baba yangu.Mama yangu hakuwa na uwezo wa kunitunza hivyo basi sikuweza kumjulisha mtu yeyote kuhusu tatizo langu; hata mama yangu sikumwambia".
Binti huyo alidai kuwa baba yake alimkataza kwenda kanisani kwa kuhofia kuwa angeweza kuwajulisha baadhi ya viongozi wa kanisa vitendo alivyokuwa akifanyia bintiye.
Siku ya Ijumaa Agosti 23, 2013 msichana huyo alidai kuwa baada ya yeye kurejea kutoka shuleni baba yake alitaka wafanye nae s * x lakini yeye alikataa na ndipo baba yake kwa hasira akaamua kakusanya vitu vyote vya shule ikiwa ni pamoja na sare za shule, vitabu na madaftari na kukaa navyo.
"Baada ya kufanya hivyo akawa ananilazimisha kufanya s * x ndipo nilipoamua kukimbilia kwenye nyumba ya jirani na huko ndipo nilipo vunja ukimya na kuweka wazi kitendo alichokuwa akinifanyia.
Ndipo wasamalia wema walipoamua kuzifikisha taarifa hizo katika shirika linalo jihusisha na maswala ya Unyanyasaji wa Majumbani na Waathirika Support Unit (DOVSSU) na ndipo wafanyakazi wa shilika hilo walipo amua kumtia mbaroni baba huyo na kumuweka chini ya ulinzi wakati uchunguzi zaidi unasubiriwa.
Pia, fomu kwajili ya matibabu zilitolewa kwa msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 ili aweze kuhudhuria hospitali kwa matibabu zaidi baada ya mshitakiwa kukamatwa.
0 comments:
Post a Comment