Jonah
Pounazarian ni miongoni mwa watu 100 nchini Marekani wanaougua ugonjwa
unaojulikana kwa jina la GSD-Glycogen Storage Disease Type 1B.
Miaka ya 1980’s ugonjwa huo kwa
walioupata walifariki wakiwa na umri wa miaka 2.
UKISTAAJABU
YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI…
Dylan Siegel ni mtoto mwenye
umri wa miaka 6 ambaye ni rafiki wa ukweli wa Jonah. Dylan anataka kumsaidia rafiki yake awe
katika hali nzuri na kuandika kitabu cha matumaini ambacho kitawaingizia
mamilioni ya dola kupata matibabu.
Dylan amekipa jina kitabu hicho
kuwa ni “Chocolate Bar” ambacho kilichukua muda wa saa moja kukiandika na
kukitafsiri.
Jina hilo ambalo kitabu hicho
kimepewa limetokana na watoto wa kiume (wavulana) kulitumia nchini Marekani
wanapotaka kuwasilisha ujumbe wao katika masuala ya kustaajabisha ama kuogofya.
Wazazi wake walitii na kutoa
katika machapisho katika kichapishio(printer) cha kawaida nakala 200 ambazo
waliziuza katika shule.
Baada ya kufanikisha hivyo
Debra alikuwa na mataumaini kwamba watauza nakala walizotoa. La kustaajabisha
ni pale walipoanza kuuza kitabu hicho ndani ya saa chache wakawa wamejikusanyia
kiasi cha Dola 6000 (sawa na TZS 9,600,000/=).
Baba wa Dylan, David alisema
kuwa waliamua kutoanakala kwa mara ya pilii na kuiweka katika FACEBOOK na
baadaye katika mtandao .
David aliongeza kusema watu walianza kusikia na kukihitaji kitabu
hicho na hivyo kufikia Malengo ya mtoto wao Dylan aliyowaomba wamsaidie ili
rafiki yake aweze kupona.
Miezi 6 baadaye kitabu “CHOCOLATE
BAR” kilikusanya kiasi cha dola 200,000 (sawa na TZS 320,000,000/=).
GSD ni ugonjwa amabao hushambulia
sana Ini, na kwamba Mtoto Jonah hujikuta akishindia cornstarch kama chakula
pekee ili kuendeleza uhai wake.
Lora Pournazarian alikaririwa
akisema huwa wanachanganya na maji na kumnyesha ili kusababisha damu ya Jonah
kuendelea kuwa na sukari.
Jonah aliruhusiwa kula vyakula
vingine lakini kiwango cha sukari kimekukwa kikiangalia.
Mapacha Jonah na kaka yake Eli
wanajisikia fahari kwa kitu ambacho rafiki yao Dylan amekifanya kwao kwa ajili
ya kuokoa maisha ya Jonah.
Daktari Weinstein ambaye ni
mtafiti wa magonjwa likiwemo GSD amesema
sio wote wanaolifahamu gonjwa hilo lakini pia akapigia nara kitabu cha
CHOCOLATE BAR kitachangisha fedha kwa
ajili ya kuweka uelewa kuhusu GSD.
Daktari huyo amekiita kitabu
hicho “DYLAN’S EFFORTS’’ (yaani Jitahada wa Dylan).
Jonah na Dylan kwa mara ya
kwanza walikutana shuleni wakiwa na umri wa miaka 3 katika Chekechea moja
nchini humo na mpaka sasa hawajaachana na kwamba urafiki wao utadumu.
CHANZO:
BROKEN DAILY NEWS/HLNTV.com/TODAY.com
0 comments:
Post a Comment