Kujiuliza ‘’KWANINI’’ unapotafuta ufumbuzi wa tatizo ni njia
moja wapo ya kukusaidia kutatua tatizo au kukusogeza karibu na chimbuko la
tatizo. Utumiaji wa KWANINI umewasaidia watu wengi kujua chimbuko halisi la
matatizo yao na kwa kujua hivyo wamekuwa wakitatua mambo mbalimbali na
kufanikiwa.
Unapopatwa na tatizo ukijiuliza kwanini huzaa swali lingine
la kwanini hatimaye utasogea karibu na
kujua ‘’Nini kilisababisha tatizo husika.”
Hebu tuangalie faida za kujuiliza swali hili kwanini.
- Kujiuliza kwanini kutakusaidia kutambua kiini au mzizi wa tatizo.
- Kujiuliza kwanini ni rahisi kujifunza na kuelewa tatizo lako hatimaye kukusaidia kujua mbinu sahihi ya kutumia kutatua tatizo hilo.
Na sasa namna ya kutumia mbinu hii ya kutatua tatizo.
-Unapoendea kutatua tatizo anza kuangalia mwisho wa tatizo ambao ni
matokeo ya tatizo lilipotokea kurudi nyuma kwa maana ya kuelekea mwanzo wa
tatizo kwenye mzizi wa tatizo. Rudia kujiuliza ‘’KWANINI’’ ukiendelea kutafakari
sababu mbalimbali za tatizo lako mpaka hatimaye ukaribie kiini cha tatizo.
-Ifuatayo ni mifano ya kuonyesha ni jinsi gani kujiuliza
KWANINI kunasaidia kutatua matatizo mbalimbali.
1. Mfano wewe ni mfanyabaiara, unajiuliza kwanini wateja
wako wanapungua siku hizi? Unagundua ni kwasababu hutoi huduma nzuri
kwa wateja
wako kama walivyotegemea kuhudumiwa. Baada ya kujua sababu ya tatizo
unaamua kuboresha biashara yako kwa kuwajali wateja na kukua tena
kibiashara.
2. Mfano wewe ni mfanyakazi
ofisini, unajiuliza kwanini hamkuweza
kumaliza kazi ndani ya muda mliokubaliana? Unagundua kazi ilichukua
muda mrefu
kumaliza tofauti na mlivyotegemea. Mnaamua kuanzia sasa kazi zote za
kiofisi ambazo zina uharaka na ni muhimu lazima zipangwe mapema na
kukadiriwa uzito wake kiutendaji na kuzingatia muda ili kuepusha kuvunja
makubaliano yenu.
3. Mfano wewe ni mwanafunzi, unajiuliza kwanini haukufanya
vile? Unagundua ni kwasababu haukupanga ratiba yako vizuri na kujua nini cha
kufanya wakati huo. Baada ya kujua sababu unaamua kuwa kila kazi utajiwekea malengo na kufanya mambo yako kama inavyotakiwa.
4. Mfano wewe ni mkulima, unajiuliza kwanini ulikadiria
vibaya ukubwa wa kazi? Unagundua ni kwasababu ulifanya makadirio ya
haraka ya
eneo ulilotegemea kulima hivyo hukumaliza ndani ya muda uliopanga.
Unaamua kazi zote zitakazofuata ni lazima ufanye makadirio sahihi ya
namna utakavyofanya na kuzimaliza kwa wakati.
Mpendwa msomaji kuna njia nyingi sana za kutumia katika
utatuzi wa matatizo, leo tumeona ni jinsi gani ''KIJUILIZA KWANINI'' kunasaidia kujua na kuelewa vizuri matatizo. Kujua mbinu zaidi endelea kusoma Life Skills Blog.
Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu,
tafadhali usisite kutoa maoni yako!
0 comments:
Post a Comment