Watoto Noah na Cannor Barthe wakiwa na mama yaoMandy Trecartin
Watoto
wawili wa kiume wanaotambulika kwa majina ya Noah Barthe mwenye umri wa
miaka mitano(5) na kaka ake Cannor Barthe mwenye umri wa miaka
saba(7)wameuawa baada ya kushambuliwa na nyoka aina ya python.
Watoto
hao walishambuliwa na nyoka huyo wakati walipokuwa wamelala katika flat
ya rafiki yao katika mji wa Campbellton nchini Canada.
Watoto hao walikuwa wamelala sebuleni,wakati wanapata shambulio la nyoka huyo jana asubuhi.
Mnyama
huyo ambaye alikimbia katika sehemu ya kuuzia wanyama inayoitwa Reptile
Ocean pet store ambayo inamilikiwa na rafiki wa familia Yao bwana Jean
Claude Savaie,ambayo ipo ghorofa ya chini ya jengo ambalo watoto Yao
walikwenda kulala.
Bwana
Savoie amelimbia Global News kwamba aliona kitu cha kutisha asubuhi saa
kumi na mbili asubuhi wakati anakwenda kuwaangalia watoto hao.
''Nilifikiri
wamelala lakini nikaona tundu juu ya paa,na kila kitu kilikuwa
kimeshatokea,nikawasha taa na nilichokiona ni kitu cha kutisha sana na
siamini Kama ni kweli''alisema bwana Savoie
Mama wa watoto hao Mandy Trecartin, ambae anaishi karibu na duka hilo la kuuzia wanyama la Reptile Ocean store.
Polisi
wamesema nyoka huyo anaetambulika kama Afican rock python aliingia
katika juu ya ghorofa hilo kupitia store mbili za ghorofa hilo.
Uchunguzi wa awali wa polisi unasema python alifanya shambulio hilo baada ya kutoroka katika duka Hilo la kuuzia wanyama.
''Inaonaoneka
nyoka huyu aina ya African python alipanda juu ya ghorofa kupitia
store,na ninaamini watoto hawa walipata tabu sana kwa kushambuliwa na
nyoka huyu.alisema Msemaji wa polisi
Nyoka huyo aina ya Afican rock python amepatikana kwa uchunguzi zaidi.
0 comments:
Post a Comment