Maandamano kulaani vitendo vya ubakaji. |
Mwandishi-mpigapicha ambaye alibakwa na kundi la wanaume watano mjini Mumbai amesema anataka kurejea kazini mapema iwezekanavyo.
Akizungumza kutoka kwenye kitanda chake hospitalini, manusura huyo mwenye umri wa miaka 20 ametuma meseji ya kutojali na matumaini kwa kusema 'kubakwa sio mwisho wa maisha'.
"Nataka adhabu kali kwa wote waliotuhumiwa na kutaka kuungana kazini mapema iwezekanavyo," alieleza.
Madaktari wameshasema mwanamke huyo ameonesha 'uimara mkubwa wa kiakili' tangu shambulio hilo la ubakaji lililotokea Alhamisi.
Shambulio hilo lilitokea kwenye kiwanda kilichotelekezwa huko Lower Parel, wilaya ya zamani ya viwanda ambayo sasa ni moja ya miji inayokua kwa kasi yenye majumba ya kifahari, maduka makubwa na baa.
Kesi hiyo imetonesha vidonda vya kumbukumbu mbaya ya shambulio la Desemba la kubakwa kwa mwanafunzi wa chuo kikuu na kufa katika mji mkuu wa India ambalo lilitikisa nchi hiyo.
Mwanamke huyo alikuwa ametumwa kazi akiwa na mwenzake wa kiume kupiga picha za kiwanda hicho usiku wa jana yake ndipo wanaume watano walipowavamia wawili hao.
Baada ya mwanzoni kumsaidia mwanamke huyo kupata kibali cha kupiga picha ndani ya jengo hilo, wakamgeuka na kumshambulia wakimtuhumu mwenzake wa kiume kwa kuhusika na matukio ya uhalifu mjini humo.
Alipokana kuhusika kwenye uhalifu wakamfunga mikono yake kwa kutumia mkanda na kumchukua mwanamke huyo kwenye sehemu nyingine ya jengo hilo na kumbaka kwa kupokezana, alisema Kamishna wa Polisi wa Mumbai, Satyapal Singh.
Mkuu huyo wa polisi alisema maofisa tayari wameshawakamata watuhumiwa wawili wa shambulio hilo na amewataja na kuwatambua wengine watatu.
0 comments:
Post a Comment