KUSHOTO: Kanali Muammar Gaddafi. KULIA: Tingatinga likibomoa makazi yake ya mjini Tripoli. |
Kanali Muammar Gaddafi aliamuru
kutekwa kwa wasichana wa shule ambao baadaye walishikiliwa kama watumwa
wa ngono kwenye eneo lake, kwa mujibu wa kitabu kuhusiana na dikteta
huyo.
Msichana mmoja, aliyetajwa kama Soraya, alitekwa nyara wakati akiwa na umri wa miaka 15 na kushikiliwa kwa miaka mitano katika sehemu ya chini kwenye ngome yake yenye urefu wa maili sita nje kidogo ya mji wa Tripoli.
Anasema alibakwa ovyo-ovyo, kupigwa na kudhalilishwa kwa utaratibu wa takribani kila siku na kushuhudia udhalilishaji unaofanana na huo kwa wasichana na wavulana wengine.
Stori yake na nyingine za wengine ambao wanasema walibakwa na dikteta huyo zinasimuliwa kwenye kitabu cha "Gaddafi's Harem: The Story Of A Young Woman And The Abuses Of Power In Libya" kilichoandikwa na mwandishi wa kimataifa wa Ufaransa Annick Cojean.
Kitabu hicho kimeshauza zaidi ya nakala 100,000 tangu kilipochapishwa nchini Ufaransa mwaka jana na tafsiri ya Kiingereza itakuwa mitaani mwezi ujao.
Mwandishi huyo anasema wanaume na wavulana pia walibakwa na Gaddafi pia aliwashughulikia watu maarufu na wake za waheshimiwa kutoka nchi za nje.
Kwa mujibu wa uchunguzi wake, Annick anasema walinzi wa kike ambao wamezoeleka kumzingira Gaddafi, walikuwa ni mabibi zake ambao hawakuwa na uelewa wowote wa silaha.
Annick alichunguza matumizi mabovu ya madaraka ya Gaddafi baada ya kukutana na Soraya (ambaye jina lake limebadilishwa), ambaye alimsimulia stori yake ya kuhuzunisha.
Baada ya kupeleka maua, Gaddafi, ambaye alikuwa na watoto wanane, alimpapasa kichwa chake. Alisema hii ilikuwa ni ishara kwa mikakati yake kwamba alikuwa akimtaka kimapenzi.
Siku iliyofuata aliitwa kwenye ngome yake iliyoko kwenye eneo la urefu wa maili sita karibu na Tripoli, Bab al-Azizia, ambako alivuliwa nguo zote, kunyolewa nywele na kupelekwa kwa Gaddafi.
Alisema Gaddafi alikuwa amelala akiwa hana nguo kitandani na kujaribu kumbaka.
Pale alipokuwa akimsukuma ajinasue, Soraya aliondolewa na mkuu wa nyumba ya uharimu Mabrouka kwa ajili ya 'adhabu'.
Alinukuliwa kwenye kitabu hicho akisema: "Alinikamata mikono yangu na kunilazimisha kukaa pembeni yake kitandani. Sikuthubutu kumtazama.
"Alisema, "Usiogope. Mimi ni baba yako. Hivyo ndivyo unavyoniita, sivyo? Lakini pia ni kaka yake na mpenzi wako. Nitakuwa hivyo wakati wote kwa ajili yako. Sababu utakuwa ukikaa na kuishi na mimi milele."
Mwanafunzi huyo wa kike walipewa picha za ngono kutazama na aliwezeshwa kutazama Gaddafi akifanya mapenzi na wengine hivyo kumwezesha 'kujifunza'.
Wavulana na walinzi wa kiume pia walibakwa na dikteta huyo, kwa mujibu wa kitabu hicho.
Soraya kisha akaruhusiwa kwenda nyumbani mwaka 2009 lakini anasema ameitia aibu familia yake sababu alifanya mapenzi nje ya ndoa.
Alisema alijihisi yuko huru kutoka mikononi mwa Gaddafi baada ya kifo chake mwaka 2011 mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kitabu hicho kinaelezea mahojiano na mwanamke mmoja ambaye alisafirisha wasichana hao kwenda kwenye makazi ya Gaddafi na waathirika wengine.
Annick pia anamtuhumu Gaddafi, ambaye alimuoa Safia Farkash, kutembea na wanafunzi na wake za waheshimiwa kutoka nchi za nje.
Wageni wa kike walikuwa wakipimwa damu mara kwa mara na manesi wa Gaddafi kuhakikisha hawakuwa na maradhi endapo angetaka kufanya nao mapenzi.
Marie Colvin, mwandishi wa Sunday Times aliyeuawa nchini Syria mwaka 2012, aliripoti kwamba nesi mmoja alimkabili akiwa na sindano wakati alipokuwa mjini Tripoli kufanya mahojiano na Gaddafi. Alikataa kutolewa damu.
0 comments:
Post a Comment