Saturday, 17 August 2013

WAARABU NA KUFURU YA HELA ZA MAFUTA


ROMAN Abramovich hapendi kushindwa. Kama huamini hilo waulize makocha aliowahi kuwatimua. Ni wazi hatapenda kufunikwa na Manchester City. 


Lakini bahati mbaya kwa bilionea huyo wa Kirusi hilo limetokea, hii ni baada ya Sheik Khalifa bin Zayed bin Sultan al-Nahyan kutumia kiasi cha pauni milioni 390 (sh bilioni 953.835) kununua boti kubwa zaidi duniani.

Boti ya kifahari ya mmiliki wa Chelsea, Abramovich inayojulikana kwa jina la Eclipse ndiyo ilikuwa kubwa zaidi duniani kwa miaka mitatu iliyopita, lakini sasa hivi imefunikwa na boti ya Sheik Khalifa inayojulikana kwa jina la Azzam kwa urefu wa futi 54 (mita 16.5) – ukubwa wa eneo la penalti.

Battle:
Vita: Familia ya Kifalme ya Kiarabu inatawala baharini baada ya kuibuka taarifa kwamba wanamiliki boti kubwa zaidi duniani, wamemfunika Roman Abramovich kileleni.
No expense spared: Azzam has taken one year to design and three years to build
Inaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu: Ndefu zaidi ya baadhi ya meli za maraha: Azzam inatajwa kama boti ambayo ilikuwa na changamoto kubwa zaidi wakati wa kutengenezwa.
For the playboy who has everything: Azzam the £400m superyacht blows everything else out of the water
Azzam inatoa kila kitu kwenye maji
Longer than some cruise ships: Azzam has been described as the 'most complex and challenging yacht' ever built
Ndefu zaidi ya baadhi ya meli za maraha: Azzam inatajwa kama boti ambayo ilikuwa na changamoto kubwa zaidi wakati wa kutengenezwa.

AZZAM VS ECLIPSE

Urefu wa futi 590.6, Azzam ni ndefu zaidi ya mabasi 12 ya ghorofa yakiwa yamepaki pamoja.

Sehemu pana zaidi kwenye boti hiyo inajulikana kwa jina la the beam, Azzam inaunene wa futi 68.2, wakati hull yake imeenda chini kwa futi 15.8.

Ni nzito kuliko Eclipse, inakadiriwa kuwa na uzito wa ‘gross tonnage’ 14,000GT – kwa haraka haraka ni sawa Tembo wakubwa wa Afrika 1,750.

Inaendeshwa na mapropela mawili ya gesi na injini mbili za diesel, inanguvu za horsepower 94,000 na ikiwa kwenye spidi yake ya juu kabisa inakuwa ni ‘Knots’ 30.

Tenki la Azzam linaweza kuhifadhi lita milioni 1 na kukimbia kwa mwendo wake ule ule.

Mainjia wakubwa duniani walitumia mwaka mzima ‘kuidesign’ na miaka mitatu kuitengeneza boti hiyo ya Azzam – lakini muda huu unaonekana ni mfupi sana linapokuja suala ya matengenezo.

Ndani ya boti sehemu ya futi 29 kwa ajili ya mikutano na sehemu ya wazi.

Mbunifu wa masuala ya ndani ya Meli wa Kifaransa, Christophe Leoni alitakiwa eneo la ndani la kisasa.

Eclipse ya Roman Abramovich inaurefu wa futi 533.1 na upana wa futi 72.2 na gross tonnage ya 13,500GT. Inainjini nne za diesel na kasi yake ya juu kabisa ni knots 22, hii inamaanisha kwamba Azzam inakasi kubwa zaidi kama mmiliki wake akiamua kufanya mashindano.Boti hiyo inaweza kuingiza watu 36 inaeneo la sinema, ukumbi wa mikutano, sehemu ya kuchezea watoto, saluni ya kike, sehemu ya kucheza muziki, bwawa la kuogelea na sauna.

Imetengenezwa na kampuni ya Blohm +Voss Shipyards na kubuniwa ndani ya Terence Disdale, Eclipse ilitengenezwa kwa ajili ya mmiliki wa Chelsea mwaka 2010.

Boti zote ni kubwa sana na zinaweza kushindwa kupaki kwenye sehemu nyingi za kupaki boti duniani, hata Monaco na Antibes maeneo ya Riviera boti hizo zinaweza zisitoshe.

Hatahivyo pamoja na Azzam kuifunika Eclipse sasa hivi, zote mbili zemefunikwa na Titanic kwa ukubwa. Ilitengenezwa mwaka 1912, Boti hiyo iliyozama ilikuwa na urefu wa futi 882 na upana wa futi 92.

Boti hiyo yenye urefu wa futi 590 (mita 180) inatarajiwa kuonyesha jeuri ya fedha ya mwarabu huyo miongoni mwa matajiri duniani.

Umiliki wa boti hiyo ulifanywa siri, lakini kampuni ya Yachts France, ambayo inaanda orodha ya boti kubwa duniani, ndiyo ilitoa siri kwamba inamilikiwa na rais wa Falme za Nchi za Kiarabu Emir wa Abu Dhabi. Kaka wa mmiliki wa Man City Sheikh Mansour. Ikiwa na urefu wa zaidi ya mabasi 12, Azzam siyo tu ndiyo boti kubwa duniani, lakini pia itakuwa moja kati ya boti zenye spidi kubwa zaidi. Nguvu ya horsepower 94,000 inaweza kukimbia kwa kasi ya Knots 30 au 35mph. Designer wa Kifaransa, Christophe Leoni aliambiwa abuni eneo la ndani la kisasa lenye mahadhi ya kihekalu.

Inakadiriwa kuifikia boti ya Abramovich, Eclipse, ambayo ina mabwawa mawili ya kuogelea, sehemu mbili za kutua helikopta, ukumbi, ukumbi wa sinema, nyambizi ndogo na mfumo wa kujikinga dhidi ya makombora.

Abramovich amekuwa akimiliki Eclipse, ambayo thamani yake ni pauni milioni 740, tangu mwaka 2010.

Ukubwa wa boti duniani unazidi kuongezeka wakati huu mabilionea wakichuana kumiliki boti kubwa kuliko zote duniani na waliotengeneza boti ya Azzam, (neno hilo la kiarabu maana yake dedication)  wanadai boti hiyo ndiyo kubwa na ngumu zaidi kuwahi kutengenezwa.

Ilibuniwa na Nauta Yachts na kutengenezwa nchini Ujerumani kwenye jijini la Bremen na Lurssen – iliingia kwenye maji kwa mara ya kwanza Aprili mwaka huu.

Mmiliki wa kampuni iliyotengeneza Peter Lurssen alisema; “Inawakilisha hatua nyingine kubwa kwenye historia ya utengenezaji wa baoti.”
Boti hiyo inahitaji wafanyakazi 50 na ndani inaeneo la wazi la futi 29.
 
Ilichukua cheo cha boti kubwa zaidi ya binafsi kutoka kwa boti ya Rising Sun iliyokuwa na urefu wa futi 454, inayomilikiwa na Mfanyabiashara wa Kimarekani Larry Ellison, huku boti hiyo ikichukua nafasi ya boti ya Octopus iliyokuwa na urefu wa futi 414 iliyokuwa ikimilikiwa na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft, Paul Allen.
 
“Jinsi ilivyobuniwa inaonyesha kwamba Azzam, ilitengenezwa kwa ajili ya mnunuzi kutoka Mashariki ya Kati, inavyumba vilivyojitosheleza kama 50, lakini haina sehemu kuwa ya wazi ya juu.” Alisema mpiga picha wa boti hiyo Peter Seyfferth.

0 comments:

Post a Comment