TATHMINI YAO KIMAPENZI
Kama ilivyoelezwa hapo kabla ni kwamba wao siyo watu wa kutekwa na ‘malavidavi’, isipokuwa kipaumbele chao ni kupata wanaume ambao watawafanya wawe na furaha, amani lakini juu ya yote hayo, hutaka wale watakaoshirikiana kujenga maisha.
Mara nyingi wao siyo watu wa nakshinakshi ili kuyapamba maisha ya kimapenzi, badala yake huyaacha yaende kama yalivyo. Anaweza asihoji zawadi, wala kuuliza ni kwa nini haambiwi anapendwa kama mwanzoni mwa uhusiano. Kwake kitu cha muhimu uhusiano kuwa imara.
Ukitaka kumhukumu kwa vigezo fulanifulani, kama vile ni kwa nini hakununulii zawadi, hakumbushii haki yake ya ndoa na mambo mengineyo, utakuwa unakosea. Jiulize kwamba mbona ukihitaji wewe unapata? Sasa jibu unalo kuwa yupo tayari ila haamini katika kuanza.
Kwa kawaida ni wazito mno. Wakati mwingine pirika za maisha huwafanya walale hoi kiasi kwamba hata wanapohitajika kwa ajili ya chakula cha usiku, wanakuwa wabishi. Ni vizuri kutambua na kuheshimu hisia zao. Pigia mstari kwamba wanawake wa kundi hili hawawezani na mapenzi ya kisharobaro.
Huhitaji mapenzi ya kiutu uzima. Yale ambayo yamejijenga katika sura inayotafsirika. Hisia zao hutaka huduma ya kwanza, kuziamsha mpaka zikae sawa. Zikishaamka, hutoa ushirikiano wa kiwango cha juu sana. Yale mapenzi ya kihuni, kuparamiana bila mpangilio, hayafai kwao.
Aghalabu, ni rahisi kupata malalamiko kutoka kwa wanaume wakiwashutumu wanawake wanaounda kundi hili kwamba ni wazito kitandani, hawazungushi nyonga wala hawatoi vile vilio vya kimahaba. Hii ni asili yao na huo ndiyo mtazamo wao wa kimapenzi unavyowatuma.
Wakati mwingine unaweza kudhani hawafurahii mapenzi kulingana na vile wanavyohusika faragha. Kama nawe ni mtu unayeamini zaidi kipengele cha mashamshamu ya kitandani, kwa vyovyote vile utakerwa naye. Si ajabu ukasema hana hisia na wewe.
Unaweza pia kumtuhumu kwamba anaye mwingine anayempenda ndiyo maana haoneshi hisia zenye uchangamfu kwako pindi mnapokuwa faragha. Hata hivyo, unaweza kujikuta unafanya makosa makubwa sana kuwaza hayo, kwa maana mara nyingi mwenyewe anakuwa hata hawazi mapenzi.
Hivyo ndivyo alivyo, sasa basi ili kuendana naye, hutakiwi kukasirika au kumshusha thamamani kwamba hayawezi ‘machejo’ yaliyomo ndani ya kuta nne. Unachotakiwa kutambua ni kwamba kila binadamu ana ukomo wa ubora wake. Anaweza hili na lile lakini eneo lingine ni dhaifu kwelikweli.
Wamejaaliwa sana ubora uliotukuka katika kipengele cha uaminifu, akili ya malezi, utafutaji, udhibiti wa matumizi na ujenzi wa familia makini. Ni wachache sana kukuta wanakuwa na viwango vyote hivyo, halafu na faragha wakawa wataalamu.
Weka akilini kwamba ni ngumu kumpata mwanamke ambaye atakuwa amekamilika kila idara. Wewe mwenyewe hapo ulipo una udhaifu wako. Kauli ya dhihaka: Kumpata mwenye vigezo vyote unavyotaka wewe, labda umuumbe mwenyewe.
Kitu kizuri kwako kama unataka kudumu na mwanamke wa kundi hili, uone matunda yake ndani ya ndoa yako, inakupasa kwamba uwe mvumilivu kwenye mambo madogomadogo, baada ya hapo ujifunze pia uamini katika kufundisha. Muingize darasa lisilo rasmi kwa ajili ya kumfanya ayaasili yale unayoyataraji kutoka kwa mwenzi wako.
Wakati unamwelewesha, wakati huohuo unavuta subira azoee. Usimwambie kwa ukali, kwa maana utamfanya akuone kero na atakushusha thamani, ingawa udhaifu upo kwako. Ogopa sana mwanamke akikuona wewe ni tatizo, hilo huwa linajengeka na kuishi kwa muda mrefu ndani ya kichwa chake.
Mara chache wanawake ambao huitwa akina mama wa nyumbani, kwa maana ofisi zao ni majukumu ya ndani ya familia peke yake, hujitutumua katika eneo la faragha lakini nao siyo wote. Inapotokea akazaa, ndiyo hushindwa kabisa kuonesha hata yale makeke kiduchu ambayo awali waliyaonesha.
Itaendelea wiki ijayo.
Global Publishers
0 comments:
Post a Comment