Friday, 16 August 2013

ZIJUE SABABU ZINAZOFANYA WANAWAKE WENGI KUKOSA WAUME WA KUWAOWA KWA 100%


Nimefuatilia kwa kina nakujiuliza ni kwanini wasichana wengi kuolewa imekua tabu?
Na hii ni research nimefanya kwa wasichana na vijana wa kiume ili nipate majibu sahihi.
Nimekuja kugundua matatizo ya wasichana ni mengi ndio chanzo cha wao kukosa waume.

1.
Umalaya – Ule wakati binti anaanza kuchanua badala ya kujitunza nakujiheshimu yeye ndio anatumia nafasi hiyo kuuchezea mwili wake kila mwanaume anayemtongoza anamkubali mwisho anajikuta ana maboyfriend zaidi ya mmoja, hapo anaanza kuangalia sasa maslahi na sio upendo wa dhati anajikuta kaingia kwenye wrong choice basi ataendelea kusakanyia mwengine na mwengine na mwengine ili akutane na right choice hapo kuna mabuzi kibao kuna waume za watu na vijana matapeli wote anabambana nao mwisho anashtukia yuko above 30 ana anza kulia ohh na mkosi sijui nuksi nk.

2.
Maringo – Nipale wakati binti anapokua nakujishtukia kuwa yeye ni mrembo wa ukweli, basi hapoa ataanza kujisikia kuwa yeye ni yeye kudharau wengine na kujiona babkubwa na kuwa too much selective, inapotoke kijana kampenda atakapomfata huwa anamuangalia nakumuona hana hadhi ya kuwa na yeye, itaendelea hivyoooooo mwisho atakuja kukutana na kijana mtanashati wa ukweli hapo ndio atajiaminia huyo ndio mwenye hadhi yake kumbe gubegube, mpaka aje kugundua kashaumizwa anaanza sasa kuumizwa kila mara hapo ataamua sasa kujishusha na kusarandia vijana wa kawaida, kila atakae date nae anakuta ni mchumba wa mtu au mume wa mtu au bf wa mtu, hapo ndio tayari keshakua majeruhi wa mapenzi basi itabidi aishie kuchuna mabuzi fumba na kufumbua yuko above 30 anaanza kulia nina mkosi ohh nuksi nk.

3.
Roho ya kukataliwa – samahani maana hii ipo spiritual zaidi mtaniwia radhi, kiukweli kuna watu wana roho ya kukataliwa utakuta ni msichana mrembo tabia nzuri na sifa zote nzuri anazo shida ni akwamba wachumba wanamkataa dk za mwisho, ikumbukwe huyu sio muhuni anajiheshimu na anajitambua vizuri, atapata mchumba ghafla mchumba atamtema nakwenda kwa msichana mwingine inaweza kuwa kashamvisha hata pete ya uchumba wameshatambulishana hata kwa wazazi haijalishi mwanaume atamtema tuu, hawa kwakweli ndio wanaongoza kwakujiita wana mkosi nuksi nk.

4.
Majini Mahaba – Baadhi ya wasichana wana majini mahaba kwahiyo kuolewa kwao imeshakua ni tabu anaweza apate mchumba afe au mwanaume abadilike tabia nakumchukia au mwanaume aanze kuwa Malaya na kushindwa kumvumilia hatimaye wanaachana mauzauza yanakuwa kibao kwenye mapenzi yake mwisho anajishtukia yuko above 30 anajiona ana mkosi na nuksi.

5.
Marafiki wabaya – Msichana anaweza kuwa haolewi kumbe marafiki alionao sio wema kwake, ukipata mchumba tayari umeshaenda kumweleza shosti wako au mashosti zako, bila wewe kujua wanampeperusha, watakuzunguka ,watatembea nae, watamtega, watakuongelea vibaya, watakuloga, watamloga, watakuharibia mpaka utaachwa kila mara usipokua mjanja ukashtuka ndio hivyo uanajikuta uko abave 30 unaanza kulia ohh nina mkosi sijui nuksi nk.
Mpaka hapo nina amini kwa wewe msichana ambaye huolewi kuna fungu lako moja kati ya hayo hapo juu, sasa chakufanya jitambue na ujipange upya kama ushapita above 30 usihofu sana hata miaka 60 wanaolewa bado.

1.
Umalaya – acha umalaya anza upya jitulize tubu mwombe Mungu sio uende kwa waganga, Mungu ndio
alieanzisha utaratibu wa ndoa atakusamehe na kukuhurumia na kukuletea mume wako na utayafurahia maisha.

2.
Maringo – Mungu pia anachukia maringo acha kujisikia wewe ni wakawaida sana anza sasa kujishusha na umuombe Mungu msamaha atakusamehe na kukuhurumia na atakuletea mume wako na wewe utayafurahia maisha.

3.
Roho ya kukataliwa – hii ilianza tokea tumboni kwa mamayako, mamayako akawa wa kwanza wewe ukawa wa pili kujikataa, sasa chakufanya vunja roho ya kukataliwa na uanze kujikubali vunja vunja vunja vunja roho ya kukataliwa zitavunjika roho zote na utakuwa huru kiulaini utampata mume wako na utayafurahia maisha.

4.
Majini mahaba – haya wengi wameyapata kwa waganga tabia za wasichana kewenda kwa waganga kuwaloga wanaume na kwenda kulala kwenye maguest ovyohovyo sasa anza kutubu kwanza ndio umtafute Bony Mwaitege akufanyie maombi na kujiombea mwenyewe Mungu ni warehema atakuhurumia na utafunguliwa na utakuwa huru utampata mwenzi wako na wewe utayafurahia maisha.

5.
Marafiki wabaya – Hata Mungu ametuonya sana juu ya marafiki sasa cha kufanya wewe punguza wimbi la marafiki haswa ukiwa na bf umpe nafasi yeye kuwa ndio rafiki ikibidi wakatie kamba mashosti zako kabisa na kamwe usiwahadithie juu ya mpenzi wako na kabla ya yote mwombe Mungu kwanza akusamehe na akuelekeze nini cha kufanya baada ya hapo mbona uta yafurahia maisha na mume wako Mungu atakaekupa.

0 comments:

Post a Comment