jeri Cox Chastain akikagua baadhi ya vitu vilivyokuwamo ndani ya pochi hiyo.
Vitu visivyouzika ambavyo mwanamke mmoja alipoteza kwa zaidi ya kipindi cha miaka 20 hatimaye vimerejeshwa kwake.
Pochi ya
rangi ya bluu bahari iliyoibwa Desemba, 1990 kutoka kwa Jeri Cox
Chastain, mama aliyekuwa akifanya kazi mbili wakati huo, imerejeshwa
katika himaya yake.
Msamaria mwema aliiona pochi hiyo katika paa la vigae vya jengo moja
huko Spartanburg, South Carolina, majengo kadhaa kutoka sehemu ambako
Chastain alikuwa akifanya kazi wakati huo, na kumpa kumbukumbu ya miaka
kadhaa iliyopita katika mchakato huo.
Chastain anakumbukia siku hiyo, 'siku ya malipo,' kwa uwazi. Alikuwa
akifanya kazi Hospitali ya Doctor's Memorial, ambayo ilifungwa mnamo
mwaka 1994.
Pochi hiyo ilikuwa imeibwa wakati alipotoka ofisini kwake, kabati la chuma, kwenda kununua vitafunwa.
Wakati huo aliamini kuna mtu katika jengo la ofisi yake amemuibia fedha hizo na kisha kuitupa pochi hiyo.
"Nilihisi tu ilikuwa imetupwa kwenye pipa la taka mahali fulani."
Badala yake, Chastain alipigiwa simu kutoka polisi mapema wiki hii
ikimweleza kwamba pochi hiyo aliyodhani imetoweka kabisa, imepatikana.
Shastain alikwenda kituo hicho cha polisi siku iliyofuata kuitambua pochi hiyo, ambayo ilikuwa katika 'hali safi.'
Ingawa pesa hizo zilizokuwamo, hakika, zilikwenda Shastain alifurahi
kupita kiasi kuona mlolongo wa picha na kitabu cha kumbukumbu.
Picha mojawapo kwa namna ya kushangaza ilikuwa muhimu kabisa kwa Chastain.
Ilikuwa ni picha ya kijana wake, sasa ana miaka 28, alipokuwa na
miaka mitano akiwa kavalia nguo ambazo wakati fulani zilikuwa
zikimilikiwa na baba yake.
Pia katika pochi hiyo kulikuwa na kadi za manunuzi na hata kadi za
huduma ya matibabu kwa ajili yake na mwanae, pia cheti cha kuzaliwa cha
mwanae huyo.
"Kuna mtu anawezekana kuwa alichukua [vyote hivi] na kufanya maisha mapya kwa [wao wenyewe]."
Kwa sasa Chastain ana furaha kufanya safari hii ya kumbukumbu, lakini anataka kumshukuru mtu aliyerejesha pochi yake.
Hii hakika si mara ya kwanza mtu mwaminifu kurejesha pochi iliyopotea kipindi kirefu sana.
Kutoka kwenye jengo hilo hilo, miaka michache iliyopita alirejesha pochi iliyopotea tangu mwaka 1996
0 comments:
Post a Comment