Abdul Quader Mollah
Mahakama ya Juu nchini Bangladesh imemhukumu kifo kiongozi wa kiisilamu
aliyepatikana na hatia ya mauaji ya halaiki wakati wa vita vya Ukombozi
kutoka kwa Pakistan mwaka 1971.
Mahakama hiyo ilikataa rufaa yake dhidi ya hukumu ya maisha jela na kumuhukumu kifo kwa makosa ya jinai.
Abdul Quader Mollah wa chama cha upinzani cha Jamaat E Islami
alihukumiwa maisha na mahakama maalum ya uhalifu wa kivita hapo mwezi
Fabruari.
Wakili wake amesema hii ndio mara ya kwanza hukumu ya maisha imeongezwa na kua kunyongwa.
Hukumu ya awali ilichochea maandamano ya wafuasi wa chama chake ambao wamesema hukumu dhidi ya Mollah imechochewa kisiasa.
Lakini wapinzani wake wanasema kuwa hukumu hiyo ni dhaifu mno.
Maelfu walifanya maandamano kote nchini wakitaka Mullah ambaye
alipatikana na hatia ya kuongoza mauaji ya halaiki wakati wa vita vibaya
zaidi vya kupigania uhuru anyongwe.
Maandamano hayo yalichochea bunge kufanya mageuzi ya sheria ambayo
yanaruhusu serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi wowote ulioafikiwa na
mahakama maalum ya uhalifu wa kivita nchini humo.
0 comments:
Post a Comment