Monday, 23 September 2013

Samuel Eto’o agomewa kustaafu Cameroon

etoo 9a7ba
BAADA ya kupangwa na vigogo kwenye mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia, Kocha Msaidizi wa Cameroon, Martin Ndtoungou, amesema bado wanamhesabu straika Samuel Et'o kuwa nahodha wao licha ya kudaiwa kwamba amestaafu kuichezea timu hiyo. (HM)
Eto'o aliripotiwa kuwaeleza wenzake kwamba mechi dhidi ya Libya iliyofanyika wiki iliyopita ilikuwa ya mwisho kwake kuichezea Cameroon, lakini mashabiki wengi wa timu hiyo wanaamini presha ya mchezo ndicho kitu kilichomsukuma fowadi huyo kuibuka na kauli ya kustaafu soka la kimataifa.
"Eto'o bado ni nahodha wetu wa Indomitable Lions," alisema kocha huyo.
"Hajajivua cheo chake cha unahodha, hajatueleza kwa barua rasmi. Hivyo alichokisema na wachezaji wenzake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kitabaki kuwa siri na si kitu rasmi.
"Eto'o atabaki kuwa nahodha wetu na ataitwa kucheza mechi ya mchujo dhidi ya Tunisia. Huo ndiyo msimamo wa benchi la ufundi. Chanzo: mwanaspot

0 comments:

Post a Comment