Tuesday, 24 September 2013

MAPYA YAIBUKA UTEKAJI WESTGATE SHOPPING MALL, MJANE WA KIINGEREZA AHUSIKA...

  

KUSHOTO: Samantha Lewthwaite. KULIA: Jinsi ilivyokuwa.
Shambulio la kigaidi kwenye kituo cha kibiashara Kenya lililosababisha vifo vya watu 69 liliongozwa na mjane mweupe wa Kiingereza wa mlipuaji mabomu ya 7/7, imedaiwa juzi usiku.
**Serikali jana ilirekebisha taarifa za vifo kwa kusema waliokufa ni 62 na kwamba wengine 63 hawajulikani waliko.**

Wanajeshi walisema mwanamke mweupe aliyevalia ushungi alikuwa akiwaamuru watu wenye silaha kwa Kiarabu wakati wa mauaji ya umwagaji damu ndani ya Westgate Shopping Mall mjini Nairobi.
Kundi la kigaidi la Kiislamu la Al Shabaab limedai kuhusika na tukio hilo ambalo Waingereza watatu waliuawa na watu wengine 175 kujeruhiwa.
Lilisema juzi usiku kwenye Twitter kwamba Samantha Lewthwaite, 'mjane mweupe' wa mlipuaji mabomu ya London 7/7, Jermaine Lindsay, alikuwa 'katika vyeo vyao' na 'mwanamke jasiri'.
Mateka 15 bado walikuwa wanashikiliwa ndani ya kituo hicho cha biashara baada ya zaidi ya masaa 24 ya umwagaji damu.
Shambulio hilo limeshuhudia wanaume, wanawake na watoto wakichinjwa kama wakishindwa kukariri Kuran au jina la mama wa Mtume Muhammad.
Pia wakijigamba kwamba Lewthwaite alikuwa pamoja nao, Al Shabaab wamedai wanaume wawili kutoka London, Liban Adam, miaka 23, na Ahmed Nasir Shirdoom, miaka 24, walikuwa miongoni mwa 'mashujaa hao watakatifu' katika shambulio hilo.
Kundi hilo linasemekana kuundwa kwa kiasi kikubwa, na kiasi kikubwa cha silaha na pia vifaa vya kuonea usiku.
Wameharibu kamera za CCTV ndani ya jengo hilo la biashara, kumaanisha hawawezi kutazamwa.
Katika wazimu wa kutisha, wameripotiwa kukata mikono ya miili ya waathirika wao na kuchoma moto sura zao kujaribu kuficha wasiweze kutambuliwa.
Wakiandika kwenye Twitter, magaidi hao walisema: "Sherafiyah Lewthwaite aka Samantha ni mwanamke [shujaa]! Tunafurahi kuwa naye katika mapambano yetu!"
Sherafiyah ni jina la Kiislamu ambalo sasa linatumiwa na Lewthwaite.
Mwingine alituma ujumbe akisema: "Mujahidina wetu wanajiandaa kufa kwa ajili yetu!"

0 comments:

Post a Comment