Sunday, 15 September 2013

SHEMEJI YANGU KANIAMBIA NIKITAKA NIZIME TAA NIKALE.....!!!

 



Wadau natumain hamjambo,
Nina rafiki yangu ambaye ni kama ndugu,tumetoka mbali sana na sasa ni kama mtu na kaka yake.jamaa yangu huyu(hajaoa) alikuwa na dem mmoja hivi lakini walishindwana kwa matatizo yao binafsi wakawa wameachana kama mwaka mmoja uliopita.

Kwa kuwa nilikuwa nishatambulishwa kwa shemej yangu huyo basi hata baada ya kuachana na jamaa yangu tukawa tunasalimiana,iko siku ananipigia na mimi kuna siku nampigia kumsalim. Tunaitana shemej.

Kuna kipindi shemej yangu huyo alikuwa na shida ya vijisent,kwa kuwa hakuweza kumwambia ex wake basi aliniambia mimi lakini nilimtonya ex kuwa mwenzake alikuwa na shida,jamaa hakutaka kumsaidia kabisa ex wake,nikachukua jukumu la kumsaidia huyo shem wangu.basi mawasiliano yakawa yapo kama kawaida kwa shem wangu huyo. Kuna siku shem aliniuliza kama wyf yupo home,nikamwambia alikuwepo lakini keshaondoka kurudi kazini kwake mkoa ana kama miez miwili sasa.

Basi shem akawa akinipigia simu hadi nyt kali kunisalimia na kunitakia usiku mwema. Mwisho wa siku shem akaniuliza nawezaje kuishi muda wote huo wakati wyf hayupo? Nikamjibu navumilia tu, akaniambia kweli huo ni muda mrefu ila endapo nitakuwa na shida yoyote yuko tayar kunisaidia,nanukuu;"nakuonea huruma shem wangu, muda huo ni mwingi sana kwa mwanaume,endapo utahitaji kampani yangu niko tayar kukusaidia kwa lolote wakati wyf hayupo,kwani hata huyo jamaa yako mi siko nae tena,hata mimi nilishapata mtu mwingine japokuwa kwa sasa hayupo,atarudi januari mwakani".

Niliingiwa na uoga sana lakini nikajikaza na kumwambia jamaa yangu kuwa ex wake kanipa ofa ya kapani yake na niitumie nitakavyo, jamaa akanijibu kuwa yeye alishamalizana nae, na hana sababu tena ya kurudiana nae, kama nina uwezo wa kutumia ofa hiyo basi niendelee nayo.

wadau hiyo ndo situation niliyonayo kwa sasa,naomba mwenye ushauri mzuri zaid na wa manufaa anisaidie

0 comments:

Post a Comment