"Mke wa ndoa inadaiwa alipanga na majambazi wamuue mumewe ili aweze umiliki utajiri alionao"
Arusha. Mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite mkazi wa Moshono, anadaiwa kutaka kuuawawa na mke wake wa ndoa ili aridhi mali.
Mwanamke
huyo alikamatwa na polisi Julai 19 mwaka huu baada ya mpango wake wa
kumuua mumewe wa ndoa kwa kutumia majambazi anaodaiwa kuwalipa Sh30
milioni kama malipo ya awali.
Inadaiwa
licha ya kutaka kumuua mumewe waliyezaa naye watoto wawili, alipanga
kumuua mtoto wa kwanza wa kiume wa mume wake aliyezaa na mwanamke
mwingine. Mtoto huyo anaishi mkoani Kagera.
"sikuamini
kama itafika siku mke wangu wa ndoa, tena ya Kikristo atafikiria
kunitoa roho kwa sababu ya mali, wakati nimempa yeye na familia yake
kila wanachohitaji duniani" alisema mwanaume huyo huku akitokwa na
machozi.
Alidai kuwa tukio hilo limempa mafundisho tofauti na alivyokuwa anafikiri awali.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alipotakiwa kuzungumzia
suala hilo hakukiri wala kukanusha kukamatwa kwa wahusika wanne wa
mpango huo, lakini alisema atatoa taarifa rasmi baada ya mahojiano na
watuhumiwa.
Taarifa
za mpango huo zinadai kuwa mwanamke huyo ktk kutimiza azma yake,
alimfuata dereva teksi mmoja eneo la Kijenge kumtafutia watu wanaoweza
kufanya mauaji hayo.
Inadaiwa
dereva huyo aliwasiliana na 'wahusika' na kuwapa mpango huo, lakini
mmoja wao hakutaka kushiriki' aliamua kufikisha suala hilo Polisi
walioweka mtego na kuwanasa.
Mhusika
huyo ambaye hakutaka kutajwa alithibitisha kushirikishwa na kulipwa Sh5
milioni, ikiwa ni malipo ya awali kati ya Sh20 milioni alizoahidiwa.
Hata
hivyo, baada ya kukwama mpango wa awali mwanamke huyo aliamua kutimiza
azma yake kwa kumtumia dereva teksi huyo huyo kumtafutia wauaji wengine.
Inaelezwa
dereva teksi huyo alifanikisha kukodisha wauaji wengine na
kuwasafirisha hadi mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya mauaji ya mtoto wa
kwanza wa kiume wa mume wake aliyezaa na mwanamke mwingine.
Baada
ya kupata taarifa hizo, Polisi waliweka mtego na kufanikiwa kuwanasa
wahusika wawili mkoani Kagera, hivi sasa wanahojiwa Kituo Kikuu Cha
Polisi Arusha.
Polisi
baada ya kuwanasa watuhumiwa hao, walianza upelelezi na kufanikiwa
kukamata mwingine na mwanamke huyo ambao hadi sasa wanaendelea kuhojiwa.
Inadaiwa
baada ya wahusika kunaswa mwanamke huyo alijaribu kutoa Sh50 milioni,
ili kuzima sakata hilo, lakini jitihada hizo ziliishia kwenye mtego wa
Polisi waliojipanga na kumnasa.
Taarifa za kunaswa kwa mwanamke huyo zilianza kusambaa mwishoni mwa wiki iliyopita, kabla ya kuthibitishwa na mumewe na Polis
0 comments:
Post a Comment