STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ..........
ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.
Mfano wa aina ya simu anazo daiwa kuiba Shilole
ISHU ILIKUWAJE?
Ndugu wa Diamond aitwaye Majaliwa Majuto ‘Q
Boy’ alidai ndiye mwenye simu hizo. Alisema miezi kadhaa iliyopita,
Shilole alikwenda nchini humo kufanya shoo ya muziki. Wakati wa kuondoka
alimpa simu tatu,Ipad, Samsung Galaxy na Blackberry ili akifika Bongo ampe Diamond lakini msanii huyo hakufanya hivyo.
“Alikuja
Sauzi kufanya shoo, wakati wa kuondoka nilimpa simu tatu amletee
Diamond lakini nashangaa hakufanya hivyo na mimi tangu nirudi Bongo
simpati, kila nikimpigia simu hapokei, leo ndiyo tumekutana hapa kwa
Diamond,” alilalama Q Boy.
DIAMOND ALIAMBIWA SIMU ANAZO SHILOLE
Alisema
awali akiwa nchini humo baada ya kumkabidhi mali hizo, alimpigia simu
Diamond na kumtaarifu kuwa ‘mzigo’ anao Shilole, akashangaa staa huyo
kujibu kwamba hajazipata wala hajamwona Shilole.
SHILOLE AJITETEA
Katikati ya mzozo huo, Shilole alijitetea
kwa kusema: Mi namdai rafiki yake fedha yangu ya shoo iliyobaki, kama
shilingi laki nane hivi ndiyo maana nikaamua kuzizuia simu za huyu (Q
Boy) hadi nimaliziwe pesa yangu.
Hata hivyo, katika sakata hilo ilielezwa
kuwa Shilole na Q Boy hawakuwa na makubaliano yoyote kuhusu shoo hiyo na
simu hizo hivyo madai ya mwigizaji huyo ni ‘usanii’ tu.
MAMA DIAMOND AINGILIA KATI KUOKOA
Zogo hilo lilipopamba moto na
kuashiria kuvurugika kwa amani, mama mzazi wa Diamond, Sanura Kasim
‘Sandra’ aliamua kuingilia kati na kuagiza suala la kudaiana simu
lifanyike kesho yake (Jumamosi) kwa vile siku hiyo haikuwa muafaka.
“Jamani! Jamani! We nani, Shilole na we
Majaliwa, naomba kwa leo muepusheni shetani kwani hapa si mahali pake,
ila kesho tutaitana na kumaliza suala hili, mimi mwenyewe
nitalisimamia,” alisema bi mkubwa huyo na kumaliza henyahenya
iliyoibuka.
JUMAMOSI YAFIKA, KIKAO VIPI?
Jumamosi, mapaparazi wetu
walifuatilia ishu hiyo nyumbani kwa akina Diamond na kuulizia ili kujua
kama kikao cha usuluhishi kilifanyika kama mama Nasibu alivyoagiza.
“Mh! Sijaona kikao chochote, kwanza Shilole
mwenyewe akipigiwa simu hapokei,” alisema ndugu mmoja wa Diamond huku
akiomba hifadhi ya jina lake.
MSIKIE DIAMOND
Juzi, Diamond alipopigiwa simu na kuulizwa kama anaijua ishu ya simu, alikubali.
Staa huyo alisema anashindwa kuingilia kati sakata hilo kwa sababu wahusika wote ni watu wake wa karibu kikazi.
“Yeah! Ishu ni kweli ipo, lakini mimi
nilijiweka kando mapema, nikamwambia dogo (Q Boy) afuatilie mwenyewe
baada ya kuona Shilole haeleweki.
“Unajua Shilole ni mwanamuziki mwenzangu,
dogo yupo ndani ya Kampuni ya Wasafi Entertainment (ya Diamond), sasa
kukomaa na ishu za simu tu nahisi itanishushia hadhi, napiga shoo za
hela nyingi halafu leo nakomaa kwa hela ndogo, inakuwa siyo,” alisema
Diamond.
SHILOLE TENA
Baada ya kuzungumza na Diamond,
Shilole alipigiwa simu na kuomba kufafanua kwa undani ishu hiyo ambapo
katika hali isiyotarajiwa, alimlalamikia paparazi wetu akidai
anapendelea katika sakata hilo.
“Nyiye mnamtetea tu yule dogo, mimi
sina tatizo, kama rafiki yake (aliyemuitia shoo Afrika Kusini) akinilipa
hela yangu nawapa simu zao,” alisema Shilole.
Msanii
huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia paparazi kuwa atatia timu
kwenye Ofisi za Global Publishers ili kuzungumzia suala hilo na
viongozi.
Baadaye Shilole alifika ofisini kwetu na
kufafanua juu ya sakata hilo ambapo alirudia kukiri kuzuia simu hizo
akidai kwamba anamdai Q Boy hivyo mpaka atakapomlipa ndiyo atampa simu
zake.
Q BOY NAYE TENA
Kwa upande wake, Q Boy alipozungumza
na paparazi wetu siku hiyo alisema amekusudia kwenda kufungua kesi
kituoni ili apewe msaada zaidi wa kisheria kwa vile simu hizo zinamuuma
hasa ukizingatia kuwa yeye siye aliyempeleka Shilole Afrika Kusini
kufanya shoo.
“Mimi leo (Jumatatu) nimebanwa sana,
kuna sehemu nakwenda na Diamond, nadhani nitamaliza jioni. Lakini kesho
(Jumanne) nitaamkia polisi kufungua kesi nione watanisaidiaje?” alisema Q
Boy.
POLISI AGUSIA ISHU
Risasi Mchanganyiko lilizungumza na
askari mmoja kutoka Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kummegea mtiririko
wote, kisha kumuuliza kama kuna kesi ambapo alijibu:
“Japokuwa mimi si msemaji wa jeshi (la
polisi), lakini ishu kama hiyo shitaka lake lipo, ni wizi wa kuaminiwa.
Unajua wengi wanadhani kuibiwa lazima mtu uwe hujui, lakini mtu akifanya
kama hivyo alivyofanya huyo msanii nani sijui (Shilole), kama ni kweli,
kosa linakuwa wizi wa kuaminiwa endapo atafikishwa polisi.”
DIAMOND, Q BOY WALIFANYA MCHEZO?
Hata hivyo, baadhi ya watu walioshuhudia sakata hilo walikuwa na maswali kibao yaliyokosa majibu.
Swali
la kwanza: Shilole alikwenda kufuturu kwa mwaliko wa Diamond na alijua
staa huyo na Q Boy ni wamoja na simu alizopewa ilikuwa amletee msanii
huyo, kwa nini alikwenda huku akijua ana msala?
Swali
la pili: Kama Shilole alikwenda akijua Q Boy hayupo Bongo, je! Si
kwamba ulikuwa mpango wa wawili hao kumwita ili wampe kibano ateme simu
zao?
Swali
la tatu: Je, ni kweli Shilole alizuia simu ili amaliziwe deni lake kwa
mtu aliyemuitia shoo Afrika Kusini au shetani alimwingia baada ya kutua
Bongo na kuamua kuzitumia hasa ikizingatiwa kuwa siku hizi mambo ya
Instagram ndiyo habari ya mjini?
0 comments:
Post a Comment