Inavyosemekana
imebaki Hice tu ambayo nayo kesha pewa dalali atafute Mnunuzi. Ofisi
nayo inapumulia mashine. kuna mazito ndani ya familia hiyo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na
kushtua Xdeejayz imeibua tuhuma nzito toka kwa familia ya Marehemu
Stiven Kanumba inayomtuhumua Mama wa msanii Flora Mutegoha kuuza mali za mwanae kisha pesa kunywea pombe na mzazi mwenzake Mama Lulu huku akiisahau familia.
Aidha
chanzo hicho kiliendelea kusema “ Haikupita muda tena ameuza gari
nyingine aina ya Mark II kwa shilingi milioni 6 kisha kula bata pesa
yote na sasa hivi ameshawapa madalali kazi ya kumtafuta mteja wa
kuimalizi Hice aliyokuwa anaitumia marehemu kwa ajili ya kazi zake za
Location” Alisema dada huyo ambae ni ndugu na Mama Kanumba na aliomba
hifadhi ya jina lake kwa usalama wake.
Habari
zaidi ziliendelea kusema kuwa tangu mama Kanumba ashinde kesi ya
mirathi hiyo ya mwanae amekuwa hana ushirikiano mzuri na baadhi ya ndugu
zake “ Yani kweli pesa inabadilisha mtu huyu mama sisi ni ndugu yetu
kabisa lakini tangu azitwae mali za mwanae basi hataki ushirikiano
wowote na sisi kwa mfano zile pesa za rambirambi ya msiba milioni sabini
akachukua milioni 50 akanunua nyumba maeneo ya Mbezi Temboni hilo
tulimpongeza” Alisema bint huyo mdogo
Msichana huyo aliongeza kusema “ Lakini baada ya hapo mama huyu
alikutana na Mama Lulu ambapo hali imekuwa mbaya ambapo wenyewe
wameshauriana nini sijuia na walianza kuiuza ile V8 ambapo pesa yote
walilia bata hadi ikaisha na hivi karibuni akaiuza gari nyingine ya
marehemu aina ya Mark II na pesa hiyo wameitafuna yote hadi imeisha na
sasa hivi anaimalizia ile Hice ambayo ndio ilikuwa tegemeo kwa ajili ya
kampuni sijui tufanyaje jamani?” Alimaiza kusema bint huyo kwa uchungu.
Baada ya kupata taarifa hizo waandishi wetu walijaza mafuta gari ya
ofisi na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mama huyo kwa ajili ya
mahojiano na kufanikiwa kufika nyumbani kwa Mama Kanumba ambapo
waandishi wetu wakiwa kamiri na kamera za siri aina ya Kalamu ambapo
waligonga geti hilo jeusi na kufunguliwa na msichana ambae
alijaitambulisha kwa jina la Husna ambae alisema kuwa yeye ni house girl
na mara baada wanahabari wetu kijitambulisha na kuomba kuongea na Mama
Kanumba msichana huyo alijibu kuwa Mama huyo alikuwa ametoka hivyo labda
waandishi wetu warudi tena kesho yake au baadae.
0 comments:
Post a Comment