Monday, 5 August 2013

WAFAHAMU MASTAA WA KIKE BONGO WANAOJIHESHIMU.

BAADHI ya watu kwenye jamii wamezoea kusikia au kuona wasanii kibao wakifanya mambo ya ajabu na kuwa na skendo za hapa na pale kama kupigana, mapenzi na kuzungumza mambo yasiyofaa lakini leo tunakuletea listi ya mastaa wanaojiheshimu kwa hapa Bongo...

SALOME NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’Ni staa wa kitambo wa filamu za Kibongo. Ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’. Thea amekuwa ni mfano wa kuigwa na kila msanii anayetaka au anayeingia kwenye tasnia ya filamu na jamii kwa jumla. Thea siyo mtu wa skendo kama walivyo wasanii wengine wa kike Bongo.
Amedumu kwenye sanaa kwa muda mrefu akianzia Kundi la Sanaa la Kaole wakati wa michezo ya runingani leo, leo amefikia hatua ya kucheza filamu zake mwenyewe japokuwa kumekuwa na malalamiko haonekani sana kama zamani.
SUZAN LEWIS ‘NATASHA’
Ni mkongwe wa maigizo ambaye ni mama wa mtoto mmoja. Natasha ni msanii mwenye heshima tele kwenye tasnia ya filamu Bongo ambapo hivi karibuni aliingia kwenye ndoa ya uzeeni kwani alikuwa hajaolewa hivyo kuamua kutimiza agizo la Mungu alilowapa wanadamu. 
Natasha hajawahi kuripotiwa na skendo yoyote kama baadhi ya wasanii walivyozoeleka kuwa kila siku ni watu wa matukio ya ajabu.
ILLUMINATHA POSHI ‘DOTNATA’ 
Dotnata ni staa wa maigizo, muziki na ni mjasiriamali. Ni mama asiyekuwa na skendo na hivi sasa ameokoka na amekuwa akiwashauri wasanii mbalimbali wabadilike lakini jitihada hizo zimekuwa zikigonga mwamba kutokana na wengi wao kutosikiliza ushauri wake.
Wengine humsikiliza na kumwambia asubiri kwanza wamalize starehe zao.
WASTARA JUMA 
Ni mwigizaji ambaye ni mke wa aliyekuwa msanii wa filamu za Kibongo, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’. Wastara amekuwa ni mfano wa kuigwa na wanawake wote ulimwenguni na siyo wa filamu pekee.
Wastara ni mchapakazi, hana muda wa kukaa na kufanya mambo yasiyofaa kama kuendekeza wanaume, majungu na kupigana kama ilivyo kwa wengine.

 
RIYAMA ALLY
Mwanadada wa filamu za Kibongo anajiheshimu na amejaliwa kuwa na mtoto mmoja wa kike. Hajawahi kuripotiwa na skendo. Mara nyingi yupo bize na kazi zake na huwezi kukutana naye kwenye kumbi za starehe usiku au katika makundi yasiyofaa.
Kwenye filamu Riyama anakubalika kutokana na uigizaji wake wa kiuhalisia zaidi.
YVONE-CHERRY NGATIKWA ‘MONALISA’ 
Huyu ni mtoto wa Natasha ambaye kafuata nyayo za mama yake katika tasnia ya filamu Bongo. Monalisa ni mama wa watoto wawili. 
Hana skendo na anajiheshimu na kujielewa yeye ni nani katika jamii.

0 comments:

Post a Comment