Maambukizi katika njia ya
mkojo au katika kibovu cha mkojo, tatizo hili SI miongoni mwa magonjwa ya zinaa
(STDs)
Mara nyingi tatizo hili husababishwa na
bacteria anajukanae kama E.coli,
JINSI UNAVYOENEA
UTIs ni tatizo miongoni mwa watu hasa wanawake hasa wenye
uke kwa sababu ya uwazi wa urethra kuwa karibu sana uke na tundu la haja kubwa.
Kuna bacteria hatari kutoka tumboni na
kuingia katika njia ya mkojo urethra kwa kuwafuta au kuwapangusa kutoka kwenye huo
uwazi wa uke na tundu la haja kubwa.
Vile vile watu wenye uke
(wanawake) wana mrija mfupi sana wa
urethra (mrija wa mkojo) hivyo kwa sababu hiyo ni rahisi kwa bacteria kusafiri
na kuingia kwenye kibovu cha mkojo na kusababisha maambukizi.
Kibofu cha mkojo (bladder) ni kiungo
ambacho hutunza mkojo kabla ya mkojo kuingizwa kwenye mrija urethra wake ili
utoke njekwa njia ya kukojoa.
NINI
DALILI ZAKE
Dalili za maambukizi katika njia ya
mkojo (UTIs) kama yafuatayo;
Kukojoa mara kwa mara kusiko kawaida;
Maumivu kama ya kuwaka moto wakati wa
kukojoa (kama unaunguzwa na mkojo);
Mkojo kutoa harufu isiyo ya kawaida;
Mkojo kuwa na hali ya damu ndani yake;
maumivu ya tumbo la chini mara
nyingine;
JINSI
UCHUNGUZI UNAVYOFANYIKA.
Mara zingine uchunguzi wa haya Maambukizi katika njia ya Mkojo yana unaweza kufanyika kwa kuchunguza dalili hizo nilizo taja hapo juu.
Mara zingine uchunguzi wa haya Maambukizi katika njia ya Mkojo yana unaweza kufanyika kwa kuchunguza dalili hizo nilizo taja hapo juu.
Vile vile huweza kufanyika kwa kupima
Mkojo, mkojo kupelekwa Maabara kwa uchunguzi zaidi ambapo huchunguzwa kwa
kupima kuwepo kwa Bacteria wasababishao maambukizi hayo (E.coli)
NINI
MATATIZO YAKE.
Endapo kama maambukizi haya ya njia ya
mkojo hayatotibiwa mapema na kimamilifu, maambukizi yanaweza kusambaa mpaka
kwenye mfumo wa mkojo wa juu (kwenye kibofu na figo kuathirika),
Na inapofikia hali hiyo ya maambukizi
basi inaweza kupelekea kulazwa hospitalini.
Pia, maumivu yanapokuwa ya hali ya juu,
hasa maumivu ya tumbo la chini, mkojo kuwa na
damu, haraka sana mwone mhudumu wa afya iwezekanavyo.
JINSI
INAVYOTIBIWA.
Maambukizi katika njia ya mkojo (UTIs)
Tiba yake ni rahisi tu ambapo
ANTIBIOTICS tu hutumika, (ni vizuri dawa hizo majina yake uende moja kwa moja
hospital ukaandikiwe na daktari kulingana na kiwango cha maambukizi kilivyo na
sababu zingine utakazokuwa nazo ndio maana sijaandika ni aina gani ya
ANTIBIOTICS zinazotakiwa).
Ni muhimu sana kumaliza dozi
uliyopangiwa hata kama dalili zote zimekwisha ni lazima umalize dozi hiyo.
Kama dalili ulizokuwa nazo hazikuisha
mpaka dozi inakwisha basi tambua ya kuwa, kuna uwezekano kuwa bacteria wamekuwa
sugu kwenye hiyo aina ya dawa uliyotumia.
Na utashauriwa kuchunguzwa upya na
kutibiwa upya.
Habari
gani kuhusu Mpenzi wako ama mwenza wako endapo wewe unapata Maambukizi kwenye
njia ya mkojo (UTIs)?
Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTIs)
sio ugonjwa wa zinaa .
Lakini kujishughulisha na Ngono
kunaweza kupelekea maambukizi haya na kumbuka mpenzi au mwenza wako hahitaji
kutibiwa.
KUZUIA
MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA MKOJO.
Unaweza kuzuia (sio kutibu)
Kwa kufanya yafuatayo;
Kunywa mpaka glass sita za maji kwa siku;
Kunywa mpaka glass sita za maji kwa siku;
Kunywa kwa wingi juisi chachu ya
Cranberry (jamii ya matunda Damu)
Kojoa kabla na Baada ya tendo la
ngono/ndoa
Jipanguse/jisafishe kwa kutoka mbele
kwenda nyuma mara baada ya kuoga au baada ya kujisaidia. (namaana wakati wa
kuchamba basi ni vyema ukajisafisha kwa kupeleka nyuma na sio mbele upande wa
uke ilipo urethra)
Vaa chupi au nguo za ndani zisizo bana
sana na hasa si vizuri kuvaa nguo za jamii ya nailoni, ni vizuri kuvaa nguzo za
ndani jamii ya pamba ni nzuri zaidi.
Oga Mara kwa Mara
Oga Mara kwa Mara
Pia,
kama unajua una Maambukizi katika njia ya mkojo basi fanya haya;
Jizuie au acha kunywa chai, kahawa,
bia, mvinyo na vitu kama hivyo vyenye jamii ya alkali ndani yake.
Jihadhari na juisi ya machungwa kwa
sababu vyote hivyo hubadilika na kuwa alkali ndani ya mwili ambayo huchangia
bacteria kukua ndani ya mwili asababishae UTIs.
Tumia vitamin C kama kichochezi asilia
cha kufanya ukojoe mara kwa mara.
Kitu kingine cha muhimu cha kuzingatia
ni kuzuia kutumia vimiminika/vinywaji.
Makala hii inalenga kukupa mwanga nini
juu ya ugonjwa huu wa maambukizi katika njia ya mkojo ili uweze kujua ni namna
gani ya kukabiliana nayo.
Endapo hali inakuwa tofauti basi wahi
kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.
0 comments:
Post a Comment