Somo hili
linaweza kukushangaza msomaji wangu, kutokana na ukweli kwamba ufanyaji
mapenzi, hauwezi kuupangia muda, lakini katika hali ya kawaida ipo tofauti
kubwa ya kufanya mapenzi, mchana, usiku, alfajiri na nyakati za joto na kelele
nyingi za wapita njia.
Utofauti
huu ndiyo unaweza kutofautisha hali ya kufurahia tendo kati ya mtu na mtu.
Hakuna ubishi kwamba watu wanaofanya mapenzi nyakati za joto, hupoteza msisimko
wa tendo si tu kwa sababu ya kuchoka haraka bali hata kwa kukinai harufu ya
jasho liwatokalo mwilini.
Sababu
hiyo na nyingine nyingi, zitokanazo na kutojua muda sahihi wa kufanya tendo la
ndoa, zimewafanya wapenzi wengi kushindwa kuridhika au kupata raha stahili
wakati wa kujamiiana na wapenzi wao, jambo ambalo linanipa sababu ya kufundisha
muda sahihi wa kufanya mapenzi ni upi?
Kwa mujibu
wa uchunguzi wangu, ambao pia ulitiwa nguvu na machapisho ya hivi karibuni
yaliyotolewa kwenye magazeti ya The Sun, Mirrow na The Express ilibainika kuwa
muda muafaka wa wapenzi kufanya tendo la ndoa na kufurahia ni kati ya 9:30 na
saa 4:30 usiku, Muda ambao zaidi ya wanawake 3,000 waliowahi kuhojiwa kwenye
utafiti ulioripotiwa na mtandao mmoja hivi karibuni walikiri kuwa ufanyaji
tendo la ndoa huwa na msisimko zaidi.
Hata
hivyo, muda huo ulikubaliwa na wengi si tu kwa sababu una utulivu wa hali na
mazingira, lakini pia ni wakati ambao hisia za mapenzi huamka kwa watu ambao
pengine walikuwa na majukumu ya kazi mchana kutwa. Ukichunguza utabaini kuwa
wanandoa wengi nyakati hizi huwa faragha na hata mafumanizi mengi hutokea kati
ya saa 3 na saa 4 usiku.
Utafiti wa
kitaalamu uliochapishwa na New Study hivi karibuni ulitoa tofauti za mawazo ya
kimapenzi kwa mwanaume na mwanamke, ambapo ukichukua takwimu hizo utabaini kuwa
kilele cha mawazo hayo lazima kifikie muda huo nilioutaja na kwa sababu
nilizozieleza hapo juu.
Inaelezwa
kwamba mwanaume hufikiria tendo la ndoa mara 13 kwa siku takribani mara 5,000
kwa mwaka tofauti na mwanamke ambaye anatajwa kufikiri mara 5 kwa siku na 1,825
kwa mwaka, mawazo ambao yote yamebainika kutekelezwa zaidi nyakati za usiku kwa
muda huo niliotaja.
Hata hivyo
wataalamu wengi walishindwa kukubaliana kwa pamoja juu ya umuhimu wa muda,
lakini waliafikiana kupitia ushahidi wa utafiti wa watu waliobainika kufanya
tendo la ndoa nyakati za saa 3 -4 usiku kiasi cha kuupa sifa muda huo kuwa
unafaa zaidi kufanya mapenzi na kupata matokeo mazuri.
Ifahamike
kuwa kinachozungumzwa katika makala haya si uwezo wa kufanya tendo la ndoa,
bali ni matokeo sahihi. Watu wengi wanaweza kulima, kufanya kazi, kufanya
biashara, kucheza na hata kusoma nyakati za joto, baridi sana na hata usiku na wakapata matokea,
lakini kitalaam litakuwepo swali
wamepata matokeo mazuri, wamefurahi sawa na wale waliochagua muda sahihi?
Huu ndiyo
ujumbe wangu kwa leo, ni vema wapenzi wakafanya uchunguzi na kufahamu ni muda
gani mzuri kwa mazingira ya kwao kufanya tendo la ndoa, vinginevyo wanaweza
kufanya lakini wakajikuta wanakinai mapema au wakapata raha kidogo.
0 comments:
Post a Comment