Saturday, 14 September 2013

BUNDI AENDELEA KULIA ARSENAL,OZIL HATIHATI LEO KUCHEZA

   

KOCHA Arsene Wenger anaweza kulazimika kuchelewa kuanza kumtumia Mesut Ozil baada ya kumsaini kwa Pauni Milioni 42baada ya kushindwa kufanya mazoezi leo kwa sababu anaumwa.
Kocha huyo Arsenal ataamua mwishoni kabisa kama atamtumia mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani katika mchezo dhidi ya Sunderland Jumamosi.
Ozil - kwa pamoja na Mjerumani mwenzake, Per Mertesacker - waliwasili makao makuu ya klabu, Colney, London asubuhi ya leo wakiwa wameathirika na hali ya hewa hivyo kuambiwa wasifanye mazoezi.
Mchezaji huyo ghali wa Arsenal atasafiri na timu kwa ajili ya mechi na Sunderland, lakini madaktari wa timu wataangalia afya yake asubuhi ya kesho kama anaweza kumudu kucheza mechi hiyo.



Homa ya Sunderland? Ozil akifanya mazoezi jana kabla ya kutakiwa kupumzika


Mesut Ozil na Per Mertesacker
Ikiwa hatacheza kesho, Ozil anaweza kuichezea kwa mara ya kwanza kikamilifu Arsenal Jumatano katika Ligi ya Mabingwa dhidi ya Marseille au katika mchezo wa nyumbani wa Ligi Kuu na Stoke Jumamosi ijayo.
Kiungo wa Czech, Tomas Rosicky pia ni majeruhi na ataukosa mchezo wa kesho kama ilivyo kwa mshambuliaji wa U21 ya Ufaransa, Yaya Sanogo, lakini wachezaji wawili wa England, Theo Walcott na Jack Wilshere wanatarajiwa kucheza pamoja na kiungo wa Wales, Aaron Ramsey

0 comments:

Post a Comment