Saturday, 14 September 2013

Bale kucheza mechi yake ya kwanza Madrid;

zGareth_Bale_74036.jpg
Mchezaji anayeshikilia rekodi ya dunia kwa kuwa mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi kusajiliwa Gareth Bale, atashuka uwanjani leo Jumamosi kwa mara ya kwanza kama mchezaji wa Real Madrid itakapokuwa ikikabiliana na Villarreal, kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti amesema .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliigharimu Real Madrid pauni milioni 85.3 kuhama kutoka kilabu ya Tottenham ya Uingereza Septemba mosi.(P.T)
Bale hajarishiriki mechi yeyote kikamilifu msimu huu kutokana na jeraha la mguu mbali na dakika 32 alizocheza Wales ilipolazwa 3-0 dhidi ya Serbia Jumanne.
Aidha kocha huyo Muitaliano amekiri atamtumia Bale kama mshambulizi wa upande wa kulia .
Bale kwa upande wake anasema angependa kuchangia timu yake itakapokuwa ikitafuta ushindi wa nne katika mechi nne dhidi ya Villarreal
Kabla ya kununuliwa kwake Bale ,nyota wa zamani wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo ndiye aliyekuwa ameorodheshwa kama mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi duniani.
Ronaldo alinunuliwa kwa pauni milioni 80 kutoka Manchester United mwaka wa 2009.

0 comments:

Post a Comment