Wednesday, 18 September 2013

MWALIMU AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME NDANI YA DARASA...

  

Diane Krish-Veeramany na wenzake watatu mara baada ya kujifungua salama mtoto wa kiume darasani.
Mwalimu wa shule ya msingi alilazimika kujifungulia ndani ya darasa pale mtoto wake alipotokeza kabla ya wakati, huku wenzake wakifanya kazi kama wakunga.

Diane Krish-Veeramany aliingia leba katika wiki 39 - siku moja kabla ya siku aliyopanga kuanza likizo ya uzazi - na dakika chache kabla ya kengele ya shule kulia Alhamisi iliyopita.
Baada ya dakika zipatazo ishirini za ufupisho, alijifungua mtoto wa kiume, Jonah, akiwa ameketi kwenye kiti cha compyuta huku akizungukwa na wasaidizi wake ambao walimzalisha mtoto huyo.
Bi Krish-Veeramany, mwenye miaka 30, ambaye pia ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi 18, Noah, aliyezaa na mumewe Vijaye, miaka 31, alisema kujifungua huko kilikuwa kitu ambacho hakupanga.
Alisema: "Kila mtu mwenye mtoto anafahamu unajaribu na kupanga mambo haya kichwani kwako lakini kila kitu kilitokea haraka mno, sikuweza kufikiria.
"Ilikuwa kikamilifu, yuko salama kabisa, niko salama kabisa, na ninashukuru sababu vinginevyo ningeweza kujifungulia kwenye kiti cha nyuma cha gari."
Bi Krish-Veeramany, mwalimu wa watoto, alisema aliwasili kazini katika Shule ya Msingi Manford, huko Hainault, kaskazini mashariki mwa London, mapema kuhudhuria Klabu ya Chai Alhamisi iliyopita.
Muda mfupi baada ya kula kipande cha mkate wa kuchoma alianza kupata msisimko wa hisia na kujihisi tumbo kukaza, lakini aliendelea kuchukulia kama kawaida.
Alisema: "Ilipotimu takribani Saa 2:20 asubuhi nikamtumia meseji mume wangu kusema sijisikii vizuri. Kisha baada ya mkutano wa wafanyakazi nikaongea na mkuu na kusema ninajihisi namna ya ajabu kidogo na siwezi kukaa shuleni.
"Mkuu aliniuliza kama nilikuwa nataka gari la wagonjwa lakini nilikataa na kusema hakukuwa na jambo kubwa. Nilikuwa natembea kuelekea upande mwingine wa shule nikiwa na msaidizi wangu ndipo nikahisi kitu fulani.
"Wanafunzi walikuwa wakijiandaa kuingia madarasani na nikasema nisingependa watoto wanione nikiwa hivi sababu sipendi kuwatia hofu hivyo tulikwenda kwenye darasa ambalo lilikuwa halitumiki."
Alisema alikaa kwenye dawati la kompyuta juu ya kiti cha kompyuta huku msisimko wake wa hisia ukiongezeka.
Sasa akiwa ameungana na wasaidizi watatu, akaendelea kukataa gari la wagonjwa, na alikusudia kumsubiria mumewe awasili hivyo kuweza kumpeleka hospitalini.
Alisema: "Nilikuwa mkaidi siwezi kujifungua mtoto kwenye sakafu ya darasa.
"Lakini dakika ishirini baada ya msisimko wa hisia kuanza na ndani ya dakika 40 za kumweleza mkuu nikajihisi rundo kiasi la furaha likiwasili."
Wenzake Sam Mustafa, Dita Gojnovci na Chris Sword walimzalisha mtoto huyo huku wakipokea maelekezo kutoka kwa daktari kwa njia ya simu.
Wakati madaktari wakiwasili mtoto huyo tayari alikuwa katika mikono ya mama yake.
Ilikuwa tu hadi baada ya kujifungua ndipo mataulo yalipokusanywa kutoka kila kona ya shule hiyo na Jonah akafunikwa kama sweta.
Zawadi za kwanza za Jonah zilikuwa nepi na mavazi zilizopatikana kutoka kwenye duka moja ya jirani.
Mwalimu Mkuu Tina Jacobs alisema: "Tulipiga simu kuita gari la wagonjwa lakini kabla ya kufika hapa akawa ameshajifungua ndani ya darasa tupu kwa msaada wa wasaidizi watatu wa darasa. Ilifanyika haraka mno.
"Wasaidizi hao watatu wa darasa walikuwa wenye akili sana na nimetunuku vyeti na medali katika mkusanyiko wa Ijumaa."

0 comments:

Post a Comment