Wednesday, 25 September 2013

MWANAMICHEZO MKENYA AKAMATWA NA KUHUSISHWA NA UGAIDI WA NAIROBI

  

VISA (KULIA) AKIWA KAZINI
Hata hivyo, Wakenya wengi amepinga kutumia mitandao wakitaka mchezaji raga huyo, Visa Oshwal aachiwe huru.
Oshwal alijitokeza kuwa kati ya watu waliokuwa wakisaidia walioumia kutokana na tukio la kigaidi katika jumpa la biashara la Westland jijini Nairobi.
Lakini ghafla, askari wa usalama wakamkamata wakihofu huenda alikuwa gaidi aliyejikausha na alitaka kuwakwepa kwa kutumia kigezo cha kusaidia.
Habari zimeeleza kumatwa kwa Oshwal kulitokana naye kutokuwa amevaa beji ya Red Cross, hali iliyowatia mashabiki baadhi ya polisi waliokuwa eneo hilo.

Asilimia kubwa ya magaidi wameelezwa kutoroka kama raia wema, hali ambayo imewafanya askari kuwa makini zaidi ndani na nje ya jengo hilo.

Lakini Wakenya wengi kupitia mitandao mbalimbali wamekuwa wakieleza kuwa wanamtambua vizuri Oshwal kama mchezaji mahiri wa raga.

Pamoja na hivyo wamesisitiza polisi imuachie kwa kuwa ni mtu mwema ambaye kamwe hakuwahi kuguswa au kuhusishwa hata na ugomvi wa mtaani.

Bado haijaelezwa kama Jeshi la Polisi la Kenya limeishamuachia Oshwal ambaye hata alipokamatwa alisisitiza alifika pale kwa ajili ya kusaidia.
Magaidi wa Al Shaabab wameua watu takribani 70 katika shambulizi la kushitukiza katika jumla hilo la biashara jijini Nairobi.

0 comments:

Post a Comment