Tukio alilolifanya rapper DMX hivi
karibuni la kuvua nguo na kutembea hotelini akiwa na suti yake ya asili
(utupu) inaashiria utendaji wa akili yake uko mashakani.
Katika
video iliyowekwa na TMZ inamuonesha rapper huyo aliyekuwa katika hotel
ya Detroit wikend iliyopita, kwanza alitokea upande ‘A’ wa korido ya
hotel hiyo akiwa amevaa boxer na alipofika kwenye kona ya korido hiyo
ambapo kuna mlango pembeni, alivua boxer na kukimbia kuelekea upande ‘B’
wa korido kama anafukuzwa na kitu. Baaada ya sekunde chache kupita
akapita mhudumu wa hotel mwanamke aliyeonekana akisukuma toroli lenye
vyombo, mara ghafla na DMX akarudi na mwendo ule ule mpaka pale pale
alipovulia boxer na kuivaa, kisha akaondoka akitembea kurudi upande A
alikotokea mwanzo.
TMZ walipomtafuta DMX alidai alijiskia tu kufanya alichokifanya na hajutii chochote “I’m not ashamed of anything I got”.
0 comments:
Post a Comment