Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', ambaye pia ni 
Mjumbe wa Nec CCM, Asha Baraka, akiwaka wakati akizungumza  na mtandao 
huu jana jioni alipokuwa akisimamia zoezi la kuwazuia wabomoaji 
kutobomoa nyumba na vibanda vya wananchi katika eneo hilo la Hanansifu 
bila kufikia muafaka kwa mazungumzo na wahusika. 
Zoezi hilo la kubomoa eneo hilo ili kujengwa barabara ya mtaa lilianza 
tangu mwezi wa tano mwaka huu, ambapo wenye nyumba zizizopo eneo hilo 
baada ya mazungumzo na wasimamizi wa zoezi hilo na Diwani na Mwenyekiti 
wa Serikali ya Mtaa huo, walikubaliana na kuwekewa alama eneo 
linalotakiwa kubomolewa ili kupisha upanuzi huo. 
 
 
Baada ya alama hizo ulifanyika ubomoaji na kuchimba barabara hiyo kana 
kwamba zoezi la ujenzi lilikuwa likianza muda mfupi tu baada ya 
ubomoaji, lakini cha kushangaza watu wao baada ya kubomoa waliondoka zao
 na kuacha eneo hilo likiwa na madimbwi makubwa yaliyojaa maji na 
kusababisha eneo hilo kutopitika kwa wenye magari na waenda kwa miguu. 
Aidha baada ya kumalizika kwa ubomoaji huo, wahusika wenye nyumba zao na
 fremu za maduka eneo hilo, walikaa kwa muda wa miezi miwili na 
walipohakikishiwa kuwa zoezi hilo limemalizika na hakuna ubomoaji 
utakaoongezeka, walianza kukarabati nyumba na fremu zao upya ili 
kuendelea na biashara. 
Cha kushangaza ghfla watu hao walirejea tena jana na kuchora alama mpya 
kwa kutumia mkaa, na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo jambo lililowaacha 
hoi wananchi wa eneo hilo na wenye frem zao, kutokana na kutotolewa kwa 
taarifa wala watu hao kutokuwa na kiongozi hata mmoja wa Eneo hilo yaani
 Diwani au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambao walitakiwa kuwepo ili 
kutoa ufafanuzi wa tukio hilo. 
Lakini cha kushangaza wakati wa zoezi hilo, hakuwepo Mwenyekiti wala 
Diwani, jambo lililowafanya wananchi kuhoji juu ya uhalali wa zoezi 
hilo. 
Wakati wa zoezi hilo Asha Baraka, alimpigia simu Diwani, Abasi Tarimba, 
lakini naye alimjibu kuwa hajui lolote kama Diwani na kumtumia namba ya 
simu ya mtu mwingine ili azungumze naye, wakati yeye ndiye hasa 
alitakiwa kuwapo eneo hilo na kuwatetea wapiga kura wake. 
Hata hivyo watu waliokuwapo eneo hilo walishangazwa na kitendo cha jamaa
 hao kuendelea kumoboa upande mmoja wa eneo hilo huku wakikwepa ukuta wa
 ghorofa lililopo eneo hilo ambalo ni jipya lililojengwa hivi karibuni 
kwa kukwepa gharama, wakati alama za awali zinaonyesha kuwa hata ukuta 
wa ghorofa hilo ulitakiwa kubomolewa. 
 
 
Katapila likiendelea kubomoa.... 
 
 
Asha Baraka akisimama mbele ya Frem zake eneo hilo kuwazuia jamaa hao 
kuendelea na zoezi hilo hadi upatikane muafaka na wahusika kwanza. 
 
  
 
Asha Baraka, akionyesha alama ya pili iliyowekwa jana na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo..... 
 
 
Wananchi wakimsikiliza Asha Baraka..... 
 
 
Sehemu ya madimbwi yaliyoachwa na wachimbaji hao mara ya kwanza ambayo kwa sasaa yameanza kukauka. 
 
 
Nyumba ya Asha Baraka (kushoto) inayotakiwa kubomolewa na (kulia) ndiyo 
Ghorofa lilalokwepwa ili kupindisha barabara hiyo jambo linalofanya 
kubomolewa kwa nyumba za upande mmoja. 
 
 
Asha Baraka, akionyesha alama za awali zilizowekwa kwa rangi nyekundu 
ambazo zinaonyesha kuwa hadi ukuta wa ghorofa unatakiwa kuondoka... 
 
 
Alama hiyo ipo kwenye kibanda hiki cha mkaa ambacho kipo sambamba na ghorofa hilo.. 
 
 
Alama iliypchorwa kwa mkaa mara ya pili jana....... 
 
 
Sehemu ya uhalibifu uliotokea jana wakati wa zoezi hilo.....katika moja ya fremu zilizopo eneo hilo...
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment