Tuesday, 1 October 2013

RUBANI NA MSAIDIZI WAKE WAKIRI KULALA USINGIZI HADI DAKIKA CHACHE KABLA YA KUTUA...

  

Marubani wakiwa kazini katika chumba chao.
Rubani mmoja jana amekiri kwamba yeye na ofisa wake wa kwanza walilala usingizi wakiwa ndani ya ndege ya mizigo angani - na kuamka dakika chache kabla ya kutua.

Rubani huyo, ambaye ametambulishwa kama 'John', alisema yeye na msaidizi wake walikuwa wakielekea mwisho wa zamu yao ndefu ambayo ilianza Saa 7:30 usiku wa manane.
Wawili hao walikuwa wakikaribia kutua takribani Saa 3 asubuhi nchini Hispania.
Lakini baada ya kusafiri usiku mzima, wawili hao wote wakapitiwa usingizi muda mfupi kabla ya kutakiwa kutua.
Rubani John alisema: "Tulikuwa na mfululizo mrefu wa safari kupitia Ulaya na kutua nchini Hispania Saa 3 asubuhi, muda ambao unajihisi kupungukiwa kabisa tahadhari.
"Kwa msingi, niliamka na kutazama kila kona na kugundua ofisa wangu wa kwanza alikuwa amelala pia.
"Niliamka hivyo wote lazima tulikuwa tumelala kwa kile ninachoweza kufikiri kilikuwa kipindi kifupi. Lakini bila kujali wote tulikuwa tumelala kwa kipindi kifupi wakati wa kuongoza ndege.
"Wote tulitazamana tu kila mmoja na kuhisi 'oh h ile haikuwa sawa."
Rubani huyo alifanya maungamo ya kushitua moja kwa moja katika kipindi cha BBC Radio 5 live kinachoongozwa na Victoria Derbyshire.
Mtangazaji wa radio hiyo aliuliza umbali gani ulibaki kabla ya ndege hiyo kutua pale wawili hao walipozinduka usingizini.
Rubani akajibu: "Dakika chache tu."
Victoria pia alimuuliza rubani huyo kama alikuwa akifahamu ofisa wake wa kwanza amelala kabla hajasinzia.
"Sikuwa nafahamu kwamba amelala na yeye hakuwa akijua kwamba nilikuwa nimelala."
Mtangazaji huyo kisha akauliza kama rubani huyo alifahamu ni umbali gani alikuwa amelala, kabla ya kuuliza nini ambacho kingeweza kutokea wakati wawili hao wakiwa wamelala kidogo.
Rubani John akajibu: "Hapana. Unaanguka kawaida tu - huwezi kuwa na hakika wakati unapolala kwa muda gani ulikuwa hivyo kama ni dakika 2, dakika kumi au masaa mawili.
"Tungeweza kukosa ujumbe wa waongozaji usalama wa anga kubadili uelekeo au kasi au chochote kama hicho."
Kwakuwa ndege hiyo ilikuwa ya mizigo, hakukuwa na wafanyakazi au abiria ndani wakati tukio hilo likitokea mwaka 2000.
Ndege hiyo ilikuwa ikijiongoza yenyewe wakati wote wa safari hiyo, ingawa marubani wanatakiwa kudhibiti ndege hiyo wakati ikiwa katika hali hiyo.
Rubani John aliongeza: "Inaweza kutokea kwa yeyote - bila kujali ni muda gani umekuwa safarini."
"Kama masharti mapya yataanzishwa na kutakiwa kusafiri kwa masaa marefu zaidi na kupata muda mchache wa kupumzika hali kama hii itakuwa ikitokea mara kwa mara," alisema John.

0 comments:

Post a Comment