WASICHANA
wanne kutoka Nigeria wamegundua jinsi ambacyo mkojo unaweza kutumika
kama mafuta ya kusukuma jenereta. Wasichana hao, Duro-Aina
Adebola,Akindele Abiola, Faleke Oluwatoyin na Bello Eniola, wote wenye
umri wa miaka 14 wamefanya maonyesho ya jenereta hilo na limeonekana kufanya kazi.
Genereta
hilo linaweza kufanya kazi kwa muda wa saa moja likitumia lita moja tu
ya mkojo. Linauwezo wa kuendesha vifaa vinavyotumia umeme wa kati kama
vile taa, jokofu, redio, televisheni n.k, Sasa genereta hilo
linafanyaje kazi?
Kwanza mkojo huo unawekwa kwenye chombo
kiitwacho electolytic cell, ambacho hutenganisha mkojo huo na hydrogen.
Kisha hydrogen hiyo huenda moja kwa moja kwenye chujio la maji
kwaajili ya kuisafisha na kisha kuisukuma katika gas cylinder.
Hiyo
gas cylinder nayo huisukuma hydrogen mpaka katika kitu kinachoitwa,
liquid borax ambayo huisukuma hewa hiyo na kuliwezesha jenereta kufanya kazi
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment