Friday, 26 July 2013

HAUSIGELI AZUA BALAA BAADA YA KUPANDISHA MASHETANI....ANENA MAZITO..!!




Enjoy Cleofasi akiwa chini baada ya kupandisha mapepo.
Hamida Hassan na Gladness Mallya
MSICHANA wa kazi ‘hausigeli’ aitwaye Enjoy Cleofasi (19), hivi karibuni alipandisha mapepo na kumtwanga mwandishi wa habari aliyekuwa akimhoji kuhusiana na tukio la mauaji lililotokea mjini Dodoma.

...Enjoy akitulizwa baada ya kupandisha maruhani.
Tukio hilo la kukunjwa kwa mwandishi, lilitokea juzikati Kipunguni jijini Dar wakati Enjoy alipokuwa akisimulia jinsi alivyoutoa uhai wa mtoto wa jirani wakati alipokuwa akifanya kazi za ndani mkoani Dodoma.
Wakati Enjoy akisimulia mkasa huo, ghafla  alibadilika na kuanza kuweweseka huku akionekana kama mgonjwa kisha kumkwida shati mwandishi (jina tunalo) ambaye naye alilazimika kukabana naye na kujitoa mikononi mwake.

Timbwili zito likazuka kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu waliokuwa eneo la tukio kukimbia kwa kuhofia mapepo ya msichana huyo.
Msichana huyo akisimulia alivyoutoa uhai wa mtoto wa jirani mjini Dodoma, alisema matatizo yalianza baada ya kumuona mwanamke aliyemtokea katika mazingira ya kutatanisha akiwa shuleni mjini humo.
“Mwanamke huyo alitokea kwenye maua na  kuniita huku akiniambia ametokea kunipenda na kunitaka nimfuate, nilikataa ghafla nikawa sijielewi kisha nikapoteza fahamu,” alisema msichana huyo na kudai kwamba alikuja kuzinduka akiwa ofisini kwa walimu wake akiwa hakumbuki chochote.

Baada ya tukio hilo, Enjoy alisema mwanamke huyo alimfuata tena usiku huku akiwa ananukia marashi, akiwa amevaa nguo nyeupe ilhali akiwa haonekani chini ya miguu yake na kujitambulisha kwa jina la Shakira.
 “Mwanamke huyo aliniambia kwamba yuko na wenzake, wametumwa kunichukua kwa sababu nina akili sana nikafanye kazi zao lakini nilikataa,” alisema Enjoy.
Kutokana na mfululizo wa matukio hayo, Enjoy alisema alilazimika kubadili dini na kuwa Muislamu na kupewa jina la Jamila na Shehe aliyefika nyumbani kwako kumsomea dua.
Jamila alisema baada ya kutibiwa na shehe huyo alipona na kuanza kwenda shule, safari hii akajiunga na shule ya bweni.

Aliongeza kuwa, siku moja akiwa amelala usiku alishtuka na kukiona kitanda chote kikiwa kimelowa damu kiasi cha kutisha.
Alisema alipiga kelele lakini haikusaidia kitu, walimu walipoiona hali hiyo walimrudisha nyumbani kwa ajili ya kupata matibabu.
 “Nilitibiwa na kurudi shule lakini nikiwa darasani nikawa naona giza, hivyo nikashindwa kuendelea na masomo. Nilirudi  nyumbani kisha nikapata kazi ya ndani hapohapo Dodoma huku mauzauza yakiendelea,” alisema.
Akiendelea kufanya kazi siku moja usiku alimuota tena yule mwanamke akiwa amemtokea na kumkabidhi kisu akimtaka akamuue mtoto mdogo wa jirani.
Nikiwa ndotoni niliota ninachukua kile kisu na kwenda kumchoma mtoto yule shingoni, cha ajabu wakati nikimchoma damu haikutoka baada ya hapo nikapewa kiapo nikitakiwa kuitunza siri hiyo la sivyo nitakiona cha moto,” alisema Enjoy.
Akiendelea kusimulia msichana huyo alisema kuwa, asubuhi alipata taarifa kwamba yule mtoto wa jirani aliyemuota usiku amefariki dunia kwa kuchomwa na kisu.
Kilichonishtua zaidi ni pale majirani waliposema kwamba pamoja na mtoto huyo kuchomwa kisu, damu haikuonekana hata chembe ingawa jeraha lilionekana shingoni,” alisema Enjoy kwa majonzi.
Enjoy alisema kuwa aliendelea kuitunza siri hiyo huku mauzauza yakiendelea na baada ya muda aliamua kuacha kazi na kuhamia Kipunguni Dar kwa dada aitwaye Regina Msafiri aliyeamua kumsaidia.

0 comments:

Post a Comment