Wednesday, 17 July 2013

Usafiri wa BODABODA na ufikiri mdogo wa baadhi ya Watanzania



Usafiri wa bodaboda ni usafiri ambao ni kwa kiasi kikubwa umesaidia sana kutakua tatizo la kutembea umbali mrefu kwa wananchi hasa waishio katika maeneo ambayo usafiri wa magari ni tatizo. Pamojana hayo, usafiri wa bodaboda umekuwa na manufaa makubwa kwa vijana wengi ambao walikuwa hawana kazi.
Changamoto zinazoendelea kujitokeza ni namna usafiri huu unavyoendelea kugharimu maisha ya Watanzania kila siku na wengine wengi kupata vilema vya kudumu.
Tunaweza kusema tunapambana na malaria, Ukimwi, Kifua Kikuu, dengu , n.k lakini kwa uhakika ajali za boda boda zinagharimu maisha ya watu wengi mno kila siku. Kila hospitali kubwa katika mikoa mbalimbali kuna wagonjwa wengi sana wa ajali za pikipiki. Ukipita karibu kila kituo cha polisi utakuta mlundikano wa pikipiki ambazo zimepata ajali.
Madereva wengi wa pikipiki hizi ni vijana, wengi wa vijana hawa kabla hawajapata pikipiki wakikuwa vijiweni pendine wavita bangi, sasa wamekuwa madereva kabla hawajaacha kuvuta bangi, unga. Nivijana ambao pengine wanatafuta hela ya bosi na kula kwa siku hiyo tu, hawana upeo wa maendeleo ya mbele, hawana mke wala watoto, hawana cha kupoteza.
Usafiri wa boda boda pia umeongeza tatizo la ujambazi nchini. Majambazi wengi sasa hivi wanatumia pikipiki kufanya uhalifu na inakuwa vigumu kuwakamata kwa kuwa piki piki zina uwezo wa kupenya vichochoro na kutokomea haraka.
Vijana wengi wanaonunua pikipiki kwa ajili ya usafirishaji abiria wanajikuta wanarudia umasikini tena wakiwa vilema au wanakufa. 
Kwa Mantiki hii, faida za bodaboda zinaweza kuwa ni ndogo kuliko hasara zake. Utafiti yakinifu ufanyike, usalama udhibitiwe, pikipiki zikaguliwe ubora wake, ziwekewe insurance kubwa ili kuweza kunusuru maisha na kuokoa mali.
Picha ionekanayo hapo juu inadhihirisha ni jinsi gani hali ilivyo, uelewa mdogo hata kwa abiria kukubali kupanda wanne, bila helment na mizigo juu. Hivi tukidharauliwa na walimwengu kuwa tuna upungufu wa akili au maarifa tutalaumu?

0 comments:

Post a Comment