Saturday, 20 July 2013

Mswaada wa ndoa umewasilishwa bungeni

african-wedding 30d14
Mswaada unaolenga kuoanisha sheria za ndoa nchini Kenya umewasilishwa bungeni.Baadhi ya mabadiliko yaliopendekezwa katika mswada huo ni pamoja na kuhalalisha ndoa za wake wengi mbali na kuziimarisha sheria zote saba za ndoa.
Mapendekezo mengine ambayo huenda yakazua hisia kali ni yale ya kugawa mali iliochumwa katika ndoa pamoja na adhabu ya wanaume ambao huvunja ahadi zao za kuwaoa akina dada.
hdg

Taarifa zinazohusianaKenya
Hatahivyo akina dada wana kibarua cha kuthibitisha mahakamani iwapo ahadi hiyo ilitolewa na kuvunjwa.
Licha ya kuwa ndoa za WAKE wengi hutekelezwa na jamii nyingi nchini kenya, bado hazijahalalishwa.lakini katika mswada huu mpya ,ndoa hizo zimependekezwa.Hatahivyo mwanamume ambaye angependa kuingia katika ndoa hizi ni sharti aweke wazi majina yote ya wake zake mbele ya msajili wa ndoa pamoja na rukhsa aliyopata kutoka kwa wake hao.
Vilevile wake hao pia watalazimika kutia sahihi makubaliano kwamba wako tayari kumruhusu mume wao kuongeza mke mwengine.Makubaliano hayo yatalazimika kumfikia msajili wa ndoa siku 21 kabla ya harusi hiyo.hatua hiyo inalenga kupunguza migogoro ya ndoa inayotokana na kifo cha mwanamume aliyeoa.
Hatahivyo mswada huo unashinikiza kwamba ni sharti mtu aingie katika ndoa hiyo kupitia dini ya kiislamu au sheria za ki-mila.Wale ambao wanataka kuoa au ambao wameoa kupitia sheria za ki-kristo,ki-hindu ama sheria za kawaida hawatakubaliwa kuongeza wake zaidi ya mmoja.
Mabadiliko mengine ni yale ya walio katika ndoa kugawanya mali waliochuma kwa usawa bila kujali ni nani aliyechangia pakubwa kupata mali hiyo.
licha ya mswada wa hapo awali kupendekeza kufutiliwa mbali kwa mahari ,mswada huu mpya uko wazi kuhusu hilo na kwamba mtu anaweza kulipa Mahari au la akizingatia desturi za jamii yake.Mswada huo pia unawalinda wahusika dhidi ya kulazimishwa kuoa.
Hii ina maana kwamba wapenzi walioachana wana uwezo wa kwenda mahakamani kutokana na ahadi za uwongo zilizotolewa na wapenzi wao.
Aidha wanaume au wanawake walio-ahidiwa kuolewa na ahadi hiyo kuvunjwa watahitaji kulipwa fidia.hatahivyo mwanamke atalazimika kudhihirisha mahakamani iwapo hatua hiyo ilimuathiri. Harakati za kuwasilisha mswada kama huo hapo awali zimegonga mwamba bungeni, huku wabunge wengi wa kiume wakisema kuwa unawapa wanawake uwezo mkubwa katika ndoa.

0 comments:

Post a Comment