MCHEZAJI mpya wa Barcelona,
Neymar ameanza mazoezi na timu yake hiyo mpya baada ya kukamilisha vipimo vya
afya.
Wachezaji
wote wa Barcelona waliokuwa kwenye Kombe la Mabara walitipoti jana baada ya
mapumziko na Neymar alikuwa miongoni mwao pamoja na Xavi, Andres Iniesta, Cesc
Fabregas na Lionel Messi.
Ilikuwa
mara ya kwanza kukutana na wachezaji wenzake wapya, baada ya kuweka rekodi ya
kuwa mchezaji wa pili ghali katika historia ya klabu baada ya Zlatan
Ibrahimovic mwaka 2009 kusajiliwa kwa Pauni Milioni 56.
0 comments:
Post a Comment