MTOTO
wa miaka sita amenajisiwa na kisha kuuawa kikatili kwa kukatwa shingo na mkono kwa
panga na kijana mwenye umri wa miaka 14.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai
29 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Ijoka kata ya Mpombo
wilayani Rungwe wilaya ambayo inashiriki katika kuendesha mradi wa majaribio wa
kupinga ukatili wa jinsia na watoto(GBV) unaoendeshwa na shirika la Watereed kwa
ufadhili wa watu wa marekani kupitia mfuko wa rais wa nchi hiyo.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan
Athumani alimtaja mtoto aliyetendewa ukatili huo kuwa ni Janeth Mwailima mkazi
wa Ijoka ambapo kabla ya kuawa alibakwa.
Alimtaja mtuhumiwa wa vitendo hivyo vya
kinyama kuwa Narbeth Haule anayedaiwa kuwa mkulima na mkazi wa kijiji cha Ijoka
hali inayodhihirisha alitenda unyama huo pasipokujali udugu wa kuheshimiana na
kusaidiana katika mambo mbalimbali ambao wamekuwa nao wakazi wa vijiji vya
wilayani Rungwe na mkoa wa Mbeya kwa ujumla.
Kamanda Athuman alisema awali baada ya
kubakwa mtoto Janeth aliapa kwenda kuwaambia wazazi wake akiwemo baba yake juu
ya unyama aliotendewa na ndipo kijana huyo aliamua kwenda nyumbani kwao
kuchukua upanga na kuja kumkata mtoto huyo shingoni na mkono wake wa kulia lengo
likiwa ni kupoteza ushahidi wa kubaka.
Alisema tayari jeshi hilo linamshikilia
kijana huyo na kuwa taratibu mbalimbali za kisheria zinaandaliwa ili aweze
kufikishwa mahakamani na mkono wa sheria kuchukua mkondo wake kwa roho ya ukatili
na unyama aliyo nayo dhidi ya binadamu wenzake.
CHANZO: Joachm Nyambo wa LYAMBA LYA MFIPA-Mbeya
0 comments:
Post a Comment