KWA WANAFUNZI WA CHUO MWAKA WA KWANZA
Unapoanza maisha ya chuo, sio tu ni mwaka wako wa kwanza katika masomo
na maisha mapya ya kukua kwako, bali pia ni mwanzo wa matumizi
kuongezeka. Unapo achana na wazazi na kujiunga
na chuo, ni lazima uelewe umuhimu wa BUDGET. Anza kwa kujitengenezea
budget na kuifuata - ni jambo muhimu sana na itakusaidia hata
utakapomaliza masomo na kuanza kazi.
Unaweza kuanza chuo na
‘confidence’ kwa kuwa umesha wa ‘impress’ wazazi na jamaa kwa kufaulu
vizuri, lakini, tilia maanani kuwa ‘solid habits’ za kukua kwako ni
kuishi kwa urefu wa kamba yako. Tuanze leo kuzungumzia umuhim wa budget
yetu, hebu tuangalie kwanza tuna kiasi gani cha kutumia kwa siku, kwa
wiki au kwa mwezi.
- Anza na mkopo au ‘pocket money’
uliyonayo. Kama unapewa kwa semester au kwa mwezi, basi gawanya kwa siku
30 na utapata budget ya matumizi yako kwa siku moja.
- Pesa
yeyote ya ziada unayopewa na shangazi, mjomba, kaka, nk.. ziweke benki
na usizifuje. Unaweza kuziingiza kwenye budget yako au kuzihifadhi kwa
ajili ya dharura. Usipende tabia ya kupiga simu home na kuomba pesa bila
sababu, maana tabia hii yaweza geuka kuwa ya kudumu mpaka ukubwani.
Anza kujenga ‘healthy habits’ bado mapema, ili umalizapo chuo utakuwa
tayari kukabiliana na “real world.” Jitahidi kuishi kulingana na budget
yako.
- Pendekeza wazazi au walezi wakutumie pesa mara moja kwa
mwezi na wazideposit kwenye account yako ya benki. Kama wataamua
kukutumia pesa za matumizi kwa mkupuo, mfano za miezi mitatu au sita,
unapaswa uzigawe katika budget yako vizuri.
- Kama utatumiwa
pesa kwa njia za mitandao ya simu, hakikisha ‘password’ yako umeitunza
salama na hakuna mtu anaijua. Wizi katika pesa za mtandao hutokea kwa
wingi usipokuwa makini.
- Kama una ajira ya part time huku
ukiwa unasoma, ni fursa nzuri kwako kujiwekea akiba na kuacha kutumia
pesa bila sababu. Mara kwa mara angalia akiba yako iliyobaki na malengo
yako uliyojipangia, kama umepanga kutumia Sh.3,000 kwa siku na
ukajikutua umetumia Sh.5,000 basi kesho yake jibane utumie Sh.1,000 tu.
- Kama unatakiwa kununua vitabu, bana matumizi kwa kununua 'used text
books' na sio mpya. Vifaa vya dorm au hostel hununuliwa mwanzoni,
usiache kuziingiza katika budget yako pia kabla hujaanza kutengeneza
budget yako ya matumizi kwa siku.
Vitu muhimu vya kubudget kama unaishi nje ya chuo ni kama ifuatavyo;
- Kodi ya chumba au Hostel kwa mwezi
- Matumizi ya kila siku, sabuni, chakula, nk.
- Vocha za simu
- Photocopy na printing assignments na mahitaji ya darasani
- Kwa ajili ya matibabu unapswa ujiwekee akiba kidogo kama huna ‘Bima’ ya afya
- Usafiri wa daladala. Bodaboda na bajaji utajikuta unavuka budget yako
kama hupendi usafiri wa daladala. Kama una gari lako usisahau petrol,
service na insurance.
- Usisahau kubudget na pesa za usafiri wa kwenda nyumbani chuo kikishafungwa.
- Kama ni wazazi wanakulipia kila kitu, keti nao chini ili mpange
budget kwa Pamoja kabla ya kwenda chuo kuanza masomo yako. Angalia kama
itakubidi uwe unajipikia mwenyewe au unakula nje kwa mama lishe. Kama
kuna canteen ya wanafunzi, dadisi bei ya vyakula, breakfast, lunch na
dinner ili ujipange.
- Unapo discuss budget yako na wazazi,
onyesha kuwa una nia ya kujipanga usikwame katika masomo yako na sio
kujilimbikizia pesa. Zingatia kima cha chini cha mfanyakazi na
wanawezaje kuyamudu maisha yao kwa mwezi. Hata kama wazazi wako wanao
uwezo kifedha, tabia ya kuishi kwa buget ya mwanafunzi itakufunza kuishi
katika mazingira halisi ya chuo. Budget yako ilingane na hali halisi ya
maisha na sio ku 'over budget' au 'under budget' ukajikuta unakwama.
- Unapobakiza akiba kwenye budget yako ndipo unaweza kununua nguo,
viatu au kwenda movie au gym. Hivyo vitu sio vya muhimu sana na
kuviwekea budget kila mwezi kwa sababu ukumbuke kuwa wewe ni mwanafunzi,
ukisha anza kazi utavaa kila nguo unayotamani kuwa nayo.
-
Vitu kama laptop ni muhimu kwa mazingira ya sasa, lakini isikuumize
kichwa sana mpaka ukakosa raha kama huna laptop. Kumbuka maprofesa wote
walioko chuo kikuu kwa sasa walisoma bila laptop enzi zao na walifaulu
vizuri tu. Hivyo kama kila mtu amebeba laptop kwenye bega lake na wewe
huna, usiji ‘stress’, nenda zako Library na utaona upana wa ‘knowledge’
unaokusubiri humo.
- Ukiweza kuishi maisha yako ya chuo kwa
budget bila kuomba, kufuata mkumbo au kuishiwa, utajikuta maisha yako
yamejaa furaha na muda wako mwingi uta ‘focus’ na masomo yako. Ukiishiwa
pesa utakosa raha na amani moyoni itapotea, utaanza kutamani mambo
yasiyo kuletea neema. Budget, budget, budget and stick to your budget!
Tunakutakia siku njem
2 hours ago
0 comments:
Post a Comment