Mashoga na Wasagaji wamefunga ndoa iliyoshuhudiwa na mamia
ya watu katika Kisiwa cha Rhodes Island na Minnesota jana nchini Marekani.
UKISTAAJABU YA MUSA, UTAYAONA YA FIRAUNI…
CATHY TEN BROKE NA MARGARET MILES WAKIPEANA KITU ROHO
INAPENDA MWEEE! HUKU MCHUNGAJI JAMES NA MEYA WA JIJI LA MINNEAPOLIS R.T RYBAK
Ripoti mbalimbali Agosti Mosi
mwaka huu nchini Marekani, zinasema kuwa kwa sasa nchini Marekani zaidi ya robo
ya Wamarekani wanaunga mkono ndoa za jinsia moja na makanisa mbalimbali
yameingia na kuendelea kufungisha ndoa za aina hiyo.
Usiku wa kuamkia leo (kwa saa za
Afrika Mashariki) katika Jimbo la
Minnesota kumelipuka nderemo na vifijo pale mashoga Zachary Marcus na Gary
McDowell walipobadilisha hati za viapo katika ukumbi wa Jiji wa Providence (Providence
City Hall) mbele ya Meya wa Jiji hilo Angel Taveras.
McDowell (28) mtafiti katika
Harvard Medical School aliyezaliwa Northern Ireland na kwa mujibu wa sheria za
taifa hizo kwa sasa zinampa haki ya kuweza kuishi na kuwa na makazi ya kudumu na mumewe.
Marcus (25) ambaye ni Mwanafunzi
wa Brown University akinukuriwa na vyombo vya habari nchinihumo amesema imekuwa
siku ya furaha kwake na ushindi wa kisiasa.
Majimbo 13 nchini Marekani likiwemo
la Wshington ndoa za jinsia maoja zinakubalika bila pingamizi lolote.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa
na Kundi la Haki za Mashoga na Wasagaji imesema 30% ya wakazi waliopo nchini
Marekani sasa wanaishi katika maeneo
ambayo ndoa za mashoga na wasagaji ni haki ya msingi.
Watu akali ya 1,000 hapo jana
katika Jiji la Minneapolis (Minnesota) walikusanyika katika ukumbi wa mikutano
wakisherehekea ndoa ya 46 ya watu wenye jinsi moja ikifungwa na kupewa Baraka zote
na Meya R.T. Rybak.
Gavana wa Jimbo la Minnesota Mark
Dayton ametangaza Agosti Mosi kuwa “Freedom
to Marry Day” jimbo humo.
Mawakili wamesema Sherehe za mjini
humo, zilikuwa za kufana kutokana na ukweli kwamba majimbo yaliyo karibu nayo
yamekubali ndoa za jinsia moja.
Gavana wa Chama cha Democrats,
Lincoln Chafee ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza kabisa kushabikia ndoa za
jinsia moja kisheria, alipokuwa Seneta
wa Chama cha Republican anapanga kuhudhuria kikao cha watunga sheria za ndoa za
jinsia moja.
Pia jana hiyo hiyo Cathy ten
Broeke na Margaret Miles nao wamefunga pingu za maisha wakiwa ni wasagaji wa
kwanza kabisa kufunga ndoa katika Providence City Hall.
Watunga sheria waliopo katika
Rhode Island chenye waumini wengi wa kikatoliki wamepigana kufa au kupona kwa
miaka 16 sasa hata kupitishwa kwa sheria za Mashoga na wasagaji.
WAKAZI WA MINNESOTA WAKIUNGA MKONO NDOA ZA JINSIA MOJA AGOSTI MOSI
CHANZO: AP/YAHOO News
0 comments:
Post a Comment