Wikiendi hii kutashuhudiwa mvulana mwenye
Umri wa miaka 2 kuwa BEST MAN katika harusi ya wapendao wawili nchini Marekani.
UKISTAAJABU YA MUSA, UTAYAONA YA
FIRAUNI…
Duru
za Habari kutoka katika mjini wa Jeannette uliopo katika Jimbo la Pennsylvania
nchini Marekani zinasema Wapendanao Sean Stevenson na Christine Swidorsky
walitamani kufunga pingu za maisha mwaka 2014 lakini wameahirisha sasa
watafanya siku ya Jumamosi(Agosti 3).
Hatua
hiyo imewafika wapendanao hao baada ya kuambia na madakatari kuwa “baby boy”
wao Logan wenye umri wa miaka 2 atafariki baada majuma mawili yaani siku 14
zijazo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na The San Luis Obispo Tribune imesema kuwa
madaktari wamethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa kansa Luekemia kwa mtoto Logan.
Wakinukuriwa
wapendanao hao wamesema wanamtaka Logan aonekane katika picha za familia yao,
pia Logan aone ndoa kati ya baba na mama yake ikifungwa.
Habari
hii kwa mara ya kwanza iliripotiwa na Pittsburgh Tribune Review kwamba katika
siku ya ndoa hiyo mtoto mwenye umri wa miaka 13 ambaye Swindorsky alimpata
alipokuwa katika uhusiano na mpenzi wake wa zamani atasimama kama Bridesmaid na
binti mwingine mwenye umri wa mwaka mmoja mabaye amefahamika kwa jina moja tu
la Savannah atakuwa “Flower Girl”.
Shirika
la Habari la Marekani (AP) limesema Logan alipatwa na Fanconi Anaemia ambao
mara chache sana kuweza kusababisha kansa, ambapo mwezi Machi mwaka huu
alipoteza figo yake na sasa anakabiliwa na hali tete ya figo iliyobaki.
Juma
lililopita madaktari waliwaambia wapendanao hao kuwa Logan atakuwa na majuma
yasiyozidi matatu ya kuishi hapa duniani.
Baba
wa Mtoto, Stevenson amesema itakuwa ni ngumu sana kutenda lakini akijuacho ni
kwamba atamzika mtoto wake huyo kipenzi kutokana na ukweli kwamba hawezi kuzuia
hali kama hiyo isitokee.
Mama
wa Mtoto, Swindorsky amesema anaona bahati ya kuweza kumuaga mtoto wake na
kwamba amejifunza mengi kutoka kwa mwanaye huyo aliyempenda sana lakini Mungu
amempenda zaidi.
Watu
100 wanatarajiwa kuhudhuria harusi hiyo kesho (Agosti 3, 2013).
0 comments:
Post a Comment