Kila mwananchi aliyekuwa akijadili mpango huo alikuwa anatumia lugha yake kuashiria kwamba ameker
wa iwe kwa kutukana au kudharau viongozi waliohusika kupitisha utaratibu huo.
Jambo Leo tunaona kwamba ipo mianya mingi ya kukusanya mapato ya Serikali ambayo inazembewa iwe kwa kusudi au uzembe.
Miongoni mwa maeneo ambayo tunashauri yatumike kukusanya kodi kufidia kuondolewa tozo ya laini za simu ni eneo la madini.
Tukubali kwamba hili likifanyiwa kazi kwa kuzingatia uzalendo tutafikia tunakotaka tufike tena bila mvutano wala mkwaruzano.
Hiyo inatokana na jana kupitia vyombo vya habari ilitolewa taarifa kuwa tani mbili za madini aina ya Tanzanite yanayochimbwa katika eneo la Mererani Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, husafirishwa nje ya nchi kupitia nchi jirani ya Kenya huku sehemu kubwa na madini hayo hupitishwa kwa njia ya magendo bila kufuata sheria.
Serikali katika hilo haikuona haya kukiri kuwepo wimbi hilo la utoroshwaji wa madini kupitia mpaka huo na kueleza hali hiyo inatokana na nchi ya Kenya kutumia sheria za madini za zamani kwa kuacha kutoza kodi au mrabaha kwa mauzo ya vito vya thamani au madini.
Tufanye kazi kutokana na nafasi tulizoomba tuzitumie kuwahudumia watu na si buvimbisha vitambi na kubuni mbinu za unyonyaji kwa walalahoi huku mabilioni ya fedha yakiliwa na wachache tena bila haya.
Tunapenda wepesi katika mambo mazito, nchi ambayo inashindwa kukusanya kodi haiwezi kujiendesha. Tuache uzembe, tuwajibike na tuanze kwenye sekta ya madini. JAMBOLEO
0 comments:
Post a Comment