Saturday, 3 August 2013

MNENGUAJI AJINGUNDUA KUWA MJAMZITO WA KUJIFUNGUA BAADA YA KUFIKA HOSPITALI...

Mtoto wa mnenguaji huyo, Jack Arthur.
Mnenguaji mmoja ambaye alipelekwa hospitali na mama yake wakati alipoanza kusumbuliwa na maumivu ya tumbo alipatwa na mshituko kugundua alikuwa leba na karibu kujifungua mtoto.

Jodie Smith, mwenye miaka 17, alianza kutojisikia vizuri usiku wa Jumatatu iliyopita, lakini pale mama yake Lesley, mwenye miaka 47, alipompeleka A&E saa za mapema mchana, daktari alibainisha kwamba alikuwa mjamzito na amekaribia kabisa kuwa mama.
Saa kadhaa tu baadaye, mnamo Julai 23, Jodie alijifungua mtoto wa kiume Jack Arthur, huku akiwa na mshituko Lesley alikimbia haraka kwenda kununua vitu vya mtoto huyo.
Jodie, mnenguaji hodari kutoka Carleton Glen huko West Yorkshire, hakufahamu kama alikuwa mjamzito huku akiwa hajaongezeka usito wowote.
Mama Leslie, alisema: "Bado tumebaki na mshituko mkubwa. Jodie hakuacha kutabasamu".
"Amekuwa akiendea chuoni, kwenda kazini, kuhudhuria darasa lake la unenguaji, kwenda gym, kote kama kawaida. Hakuwa mgonjwa na kuonekana tu amepungua unene wakati wote wa ujauzito."
Alisema Jodie alianza kujihisi hali mbaya kwa maumivu ya tumbo Jumatatu iliyopita jioni, wakati Leslie na mumewe Michael, miaka 43, walipokwenda matembezini jioni.
Mama Leslie alisema: "Alikuwa amekwenda kwa rafiki yake wa kiume, lakini akarejea nyumbani sababu hakuwa akijisikia vizuri.
"Nilimweleza anywe paracetamol mbili, lakini nikapata simu kutoka kwa kaka yake baadaye jioni hiyo ikisema Jodie ameendelea kudhoofika na kwamba anaumwa."
"Majira ya Saa 7 usiku alikuja na kutuamsha na nikampigia daktari, lakini walitueleza tunatakiwa kwenda kwenye zahanati ya Wakefield.
"alikuwa katika maumivu makali wakati huo nikafahamu hatuwezi kuendelea kukaa naye pale, hivyo tukampeleka hadi A&E."
Tulipofika Hospitali ya Pontefract, madaktari haraka wakagundua Jodie alikuwa mjamzito na amekaribia kujifungua, na kumhamishia Pinderfields huko Wakefield, ambako alijifungua katika saa za mapema.
Kwakuwa hakuwa akihudhuria kliniki ya ujauzito hawakuwa na uhakika alikuwa kwenye hatua gani ya ujauzito.
Bibi mpya Leslie aliongeza: "Nilikuwa kwenye supamaketi majira ya Saa 12:30 alfajiri kununua vitu vya mtoto, sababu hatukuwa tumeandaa chochote.
"Wakunga wanadhani Jack alikuwa amepitisha wiki kadhaa, na pengine kipindi kizima. Alifanyiwa ukaguzi wote na anaendelea vizuri. Hata wao bado hawaamini."
Jodie, ambaye alifanya mitihani yake ya A-Level majira haya ya joto, bado anafikiria kwenda chuoni kusomea unenguaji. Rafiki yake wa kiume, Danny Yeoman, mwenye miaka 19, alisema: "Imekuwa mshituko mkubwa, bado tunajaribu kuamini."

0 comments:

Post a Comment