Saturday, 3 August 2013

MAMA ASIMULIA MACHUNGU YA KUISHI GEREZANI NA BINTI YAKE WA MIEZI MINANE...

Khadija Shah akiwa na binti yake, Malaika.
Mwanamke mmoja wa Uingereza anayetuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin amezungumzia maumivu yake makali katika malezi ya binti yake mdogo ndani ya selo katika gereza nchini Pakistan.

Khadija Shah anasema binti yake huyo mwenye miezi minane, Malaika, ndicho kitu pekee kinachoendelea kumfanya timamu wakati akisubiria kujua kama atakabiliwa na adhabu ya kifo kwa makosa anayotuhumiwa kutenda.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 25 anayetokea Birmingham bado hajapangiwa tarehe ya hukumu, miezi 14 baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kujaribu kusafirisha dawa hizo zenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni 3.2 kwenda nchini Uingereza.
Alijifungua Malaika Oktoba, lakini baadaye akalazimishwa kurejea jela kwenye Gereza Kuu la Rawalpindi, ambako anahofia mtoto wake huyo atashambuliwa na moja ya maradhi ya kuambukiza kama kifua kikuu ambacho kimetapakaa katika gereza hilo.
"Kama Malaika asingekuwapo hapa, ningeweza kuwa mwendawazimu sababu mambo ni magumu mno," alisema Khadija. "Ananifanya nizidi kuwa imara."
Taasisi ya haki za binadamu ya Reprieve imekuwa ikiwasaidia raia wa Uingereza, lakini yeye na mtoto huyo wanaendelea kukabiliana na hatma isiyojulikana inayochangiwa na kasi ndogo ya mfumo wa sheria wa Pakistan.
"Ninaendelea kunyonyesha," alisema Khadija. "Kila miezi mitatu wafungwa nchi za nje hunipa fedha kidogo kwa ajili ya kununulia bidhaa za kawaida za chakula na nepi maalumu kwa ajili ya mwanangu, ambaye ninamweka safi.
"Anapendelea kucheza na makasha matupu ya chakula. Kwa kawaida najaribu kuweka safi mazingira yanayotuzunguka, pia."
Mwaka jana mfungwa huyo alilalamika kwamba binti yake huyo mdogo amekuwa aking'atwa mara kwa mara na mbu, amekuwa akiharisha mno na hakuwahi kupatiwa chanjo za uhai.
Watoto wake wakubwa Ibraham, miaka sita, na Aleesha, miaka mitano, walishawahi kuwa jela pamoja na mama yao, lakini wakasafirishwa kwenda West Midlands zaidi ya mwaka mmoja uliopita na hakuwahi tena kuwaona tangu wakati huo.
"Wanatamani kuniona, lakini hawawezi kuniuliza nilipo," alisema Khadija. "Ninapuuza vitu. Ninapuuza kinachonitokea."
Maya Foa wa Reprieve alisema: "Tunahofia mno kuhusu Khadija na afya ya mtoto wake.
"Kinachoendelea kusumbua mno ni kwamba Serikali ya Uingereza inakula njama katika ahadi yake - kwa kutoa msaada kwa mpango wa Pakistan wa kupiga vita mihadarati, Uingereza iko mstari wa mbele katika kusaidia kupeleka watu kwenye kusubiria kifo kwa makosa ya dawa za kulevya, wakiwamo raia wake yenyewe."
Mama huyo kijana amekana kuhusika kwake tangu wakati huo alipokamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Islamabad mnamo Mei mwaka jana.
Anadai alikubali kusafirisha mabegi madogo kadhaa kama msaada kwa mwanaume waliyekutana hivi karibuni, na hakuwa akifahamu chochote kwamba mzigo huo ulikuwa umehusisha heroin.

0 comments:

Post a Comment