TAMAA ya kua na mke na
kuitwa baba, ndiyo imemfanya shoga maarufu jijini Dar es Salaam anaye julikana
kwa jina la Othuman Hamis au Anti Asu kuamua kuvua gwanda la kua `mototo si
riziki’ na kuvaa gwanda jingine la `kidume cha mbegu’.
Anti Asu ambaye pia
ameamua kuokoka na kukiri hadharani kwamba hataurejea kamwe ushoga, inaelezwa
kwamba kwa sasa anatafuta mke wa kumz
alia watoto na ambaye atampa mapenzi ya
dhati.
Imedaiwa kwamba, hivi
karibuni Othuman alijisalimisha katika kanisa la Tanzania Assemblies of God
(TAG), lililopo Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam ambako alitubu dhambi
zake.
Sani liliamua kuingia mzigoni kufuatilia `ishu’ hiyo ambapo lilifanikiwa
kumnasa Othuman akiwa katika saluni moja ya kike iitwayo Emmy’s iliyopo
Magomeni Mapipa jijini anakofanya kazi.
Alipoulizwa kuhusiana na taarifa za
kuukana ushoga, kijana huyo alithibitisha ni kweli ameacha tabia hizo na kwa
sasa ameokoka baada ya kubadili dini kutoka kwenye uislamu na kwenda kwenye
ukristo akiitwa Amos.
``Nimeokoka kiukweli kabisa. Sitaki tena kuusikia ushoga. Nimemkaribisha mungu katika
maisha yangu. Najutia dhambi zangu na namuomba yeye (Mungu) anisimamie na
kunilinda ili nisiweze kuanguka tena,’’ alisema Anti Asu ambaye anaonekana ni
mwanaume halisi. Amesema kwamba, ameamua kuanza maisha mapya na kwamba anaishi
katika kanisa la TAG Magomeni ambako amekuwa akikesha kwa maombi.
``Mimi nilikua shoga
namba moja Tanzania baada ya marehemu Anti Kessy. Hakuna alieyekua
ananifikia.Nimevunja ndoa zaidi ya 30 na nimetembea na wanaume hata zaidi ya
200. Nimeishi kinyumba na wanaume zaidi ya 10.
Nimebwakwa na kufanya kila aina
ya ufilauni. Nani ambaye alikua ananifikia mimi? Shoga gani ajitokeze hapa. Lakini sasa
nimeachana na yote haya baada ya kubaini nilikua naitwa na Mungu. Nimeludi
kwake na ninahisi amani moyoni mwangu,’’ amesema.
Ameongeza kwamba kwa
sasa anajiandaa kuoa kwani alipima kama ana maambukizi ya maradhi ya Ukimwi na
majibu yameonyesha kwamba yupo salama.`` Nashukuru kwamba hata jogoo anawika.’’
Aliongeza kwamba sababu nyingine nyingine iliyosababisha aokoke
ni kutoka na na kuugua sana tangu alipokumbwa na tukio la kubakwa na wanaume
zaidi ya 10.
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la TAG Magomeni Mikumi Dunstan
kanemba amethibitisha kuokoka kwa Anti Asu na kusema kwamba yeye ndiye
aliyemuombea na kumkaribisha rasmi kanisani hapo.
``NI kweli Amosi (Anti Asu)
tunaye hapa.Ibada ya Jumapili iliyopita tulimuombea hadharani na alidondoka
chini. Hii ni ishara kwamba alikua na mapepo yanayomsumbua. Kanisa limempa
hifadhi ya kuishi hapawakati tunamjenga kiroho.
Pia tunamhudumia kwa mavazi na
mahitaji mengine,’’ alisema Kanemba. Aliongeza kwamba uamuzi aliofanya kijana
huyo ni wa msingi na kuwataka watu wengine ndani ya jamii wenye matatizo kama
hayo kufika kanisani hapo kupata msaada wa maombi.
``kwa yoyote anayehitaji
kumsaidia zaidi kimwili basi asisite kufika hapa kanisani. Tunaamini kuwa
kuokoka kwake kutasaidia sana kuwafanya vijana wengine wenye tabia hiyo kuokoka
pia au kuacha’’ alisema Kanemba.
moja ya habari za zamani za anti asu ambaye sasa anaitwa Amosi baada ya kuokoka.
0 comments:
Post a Comment