Friday, 13 September 2013

MHAMIAJI WA ZIMBABWE ALIYESAMBAZA UKIMWI KWA MAKUSUDI JELA MIAKA MINNE NA NUSU...

  

Mwanaume aliyemwambukiza rafiki yake wa kike virusi vya ukimwi kisha kumshauri 'kutembea ovyo' ili kusambaza virusi hivyo amehukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu jela jana.

Mtu huyo mwenye miaka 32 alimficha ukweli kwamba ana virusi vya ukimwi msichana huyo, ambaye alikuwa na umri wa miaka 16 tu walipokutana.
Binti huyo aligundua kuwa ameambukizwa virusi hivyo pale alipokwenda hospitali kuonana na daktari, wakati huo wawili hao wakiwa tayari na mtoto wa kiume mwenye mwaka mmoja.
Mara msichana huyo alipogundua kwamba ameambukizwa, mwanaume huyo akamtaka kufanya mapenzi na watu wengine ili asiwe peke yake aliyeathirika na virusi vya ukimwi.
Mahakama ilielezwa kwamba kama ilivyokuwa kwa binti huyo, mwanaume huyo alifanya mapenzi na wanawake wengine watatu bila kutumia kinga, akicheza 'kamari ya Urusi' na maisha yao.
Mmoja, mwenye umri wa takribani miaka 20, baadaye aligundulika kuwa na virusi vya ukimwi. Wanawake wengine wawili walipimwa, lakini waligundulika hawakuwa wameathirika.
Mwanaume huyo 'katili', ambaye hakutajwa kwa sababu za kisheria, alikana kuhusika na shambulio la kudhuru mwili kati ya mwaka 2006 na 2008 lakini alipatikana na hatia kufuatia kesi hiyo iliyonguruma kwa siku nane katika Mahakama Kuu ya Leicester.
Alihukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu na kuwekewa zuio la miaka 10 la kutofanya mapenzi na yeyote bila kuweka bayana kwamba ameathirika na virusi vya ukimwi.
Endapo atavunja amri hiyo, ambayo inahusisha ngono salama, anaweza kufungwa jela kwa miaka hadi mitano.
Mhamiaji huyo kutoka Zimbabwe - ambaye ana ruhusa isiyo na ukomo ya kuishi Uingereza - alikutana na msichana huyo, ambaye hawezi kutajwa kwa sababu za kisheria, mwaka 2006.
Binti huyo aliieleza mahakama kwamba miezi michache wakiwa kwenye uhusiano wao, mwanaume huyo alipendekeza wajaribu kupata mtoto.
Aliieleza mahakama 'alishangazwa' na kufikiri alikuwa 'mdogo mno' lakini akakubali sababu alikuwa amezama katika mapenzi.
Walikuwa sambamba baada ya kushika ujauzito, lakini mwanaume huyo akabadilika na kuwa 'mkorofi na mgomvi'.
Mwanamke huyo, sasa ana miaka 20, alisema kwamba baada ya kurejea chuoni kufuatia kujifungua mtoto wa kiume, mwanaume huyo akawa akiingiza wasichana nyumbani kwao wakati yeye akiwa ametoka, huku mwanaume huyo akidai kwamba walikuwa 'marafiki wa kawaida tu'.
Lakini pale mtoto wao aliotimiza mwaka mmoja, mwanaume huyo akaanza kuonesha dalili za kuambukizwa maradhi yatokanayo na ngono - ambayo alilaumu kwamba yametokana na binti huyo kutokuwa 'mwaminifu'.
Wawili hao walikwenda hospitali kwa vipimo na madaktari wakamuuliza mwanamke huyo kama alikuwa akifahamu kwamba mpenzi wake alikuwa ameathirika na virusi vya ukimwi.
Siku iliyofuata binti huyo naye akapewa taarifa za kuhuzunisha kwamba naye alikuwa ameathirika.
Mtoto wao pia alipimwa - lakini majibu yake alionekana kwamba hakuathirika.

0 comments:

Post a Comment