Tuesday, 4 June 2013

KIFO CHA MANGWAIR TUJIFUNZE KITU.


  Kwa kawida dunia ni mazoea ya watu wengi kumgeukia Mwenyezi Mungu pale ambapo hukumbwa na matatizo, Kama vifo, magonjwa, njaa na hata majanga mengine ya duniani. Huenda Mungu hupitia hayo majanga kutukumbusha kitu flani au kuutambulisha uwepo wake na umuhimu wake, Na pengine kujifunza jambo. Kuondoka kwa Albert Mangwea ni moja kati ya pigo kubwa katia tasnia ya muziki na hata taifa zima la tanzania, Alikua ni msanii aliependwa na watu na pia mkali wa free style, Muda mwingine unaweza kujiuliza ni kwa nini Mungu anawachukua watu wanaopendwa na watu?, hilo ni fumbo kubwa mana hatujui ya Mungu mengi, Kilichobaki ni sisi kujifunza kupitia pigo hilo. Tutambue Mungu yupo na tunapaswa kumuabudu mana hatujui siku yetu. Napenda kuwapa pole wana familia wote wa Cowbama pamoja na wapenz wote wa muziki. Utukufu urudi kwake alie juu.

0 comments:

Post a Comment