Ni wiki tatu zimepita tukishuhudia Eviction shows tatu zilizowapa
tiketi za kurudi makwao washiriki 6 mpaka sasa, na tumeshuhudia mshiriki
wetu Feza Kessy akiponea kwenye tundu la sindano baada ya kura za wa
Tanzania na wa Afrika kumuokoa, sasa ni zamu ya Nando ambaye yuko
hatarini wiki hii.
Big Brother jana ametaja majina ya washiriki 7 ambao wako hatarini
kutoka wiki hii na kati yao yupo kijana mpole, mtanashati, ‘handsome’
Nando anaeiwakilisha Tanzania, ikiwa ndio mara yake ya kwanza
kupendekezwa .
Washiriki wengine walipigiwa kura nyingi kutoka wiki hii ni love
birds Bolt na Betty, ambao hii si mara yao ya kwanza kupendekezwa baada
ya kuponea chupuchupu kwa mara kadhaa.
Kenya wiki hii iko salama kwa mshiriki wao mmoja aliyesalia Annabel,
japo kuwa alipendekezwa kutoka wiki hii lakini kilichomuokoa ni yeye
kuwa mkuu wa nyumba ya Diamond, hivyo amepata favor ya kujiokoa
mwenyewe na nafasi yake akampendekeza Motamma wa Botswana.
Kwa ujumla walioingia wiki hii ni Nando wa Tanzania, Natasha wa
Malawi, Oneal wa Botswana, Motamma wa Botswana, Betty wa Ethiopia, Bolt
wa Sierra Leon na Elikem wa Ghana.
Tanzania bado ina nafasi nzuri sababu washiriki wote wawili Nando na
Feza wapo mjengoni na ndio maana unakila sababu ya kumpigia kura mara
nyingi uwezavyo Nando ili aweze kubaki wiki hii.
Washiriki wawili kati
ya saba waliopendekezwa watapita kwenye mlango wa ‘EXIT’ mjengoni hapo
Jumapili hii (June 23) wakati wa Eviction Show.
0 comments:
Post a Comment