Mkuu
wa zamani wa chama cha kiislamu nchini Bangladesh Ghulam Azam mwenye
umri wa miaka 91, amehukumiwa kifungo cha miaka 90 jela baada ya
kupatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, wakati wa vita vya
kupigania uhuru wa nchi hiyo mwaka 1971.
Hukumu
hiyo imewakasirisha wakereketwa wa pande mbili, wapinzani wake ambao
walitaka anyongwe, na wanaomuunga mkono ambao wamesema kesi dhidi yake
iliendeshwa kisiasa.
Azam
ambaye alikiongoza chama cha Jamaat-e-Islami wakati wa vita vya
kujitenga na Pakistan, bado anachukuliwa kama kiongozi wa kiroho wa
chama hicho.
Serikali ya Bangladesh imekanusha shutuma za chama hicho kuwa kesi dhidi ya Azam na wenzake ilikuwa ya kisiasa.
0 comments:
Post a Comment