Saturday, 27 July 2013

NUSU YA WATU HAWAJUI KUTUMIA KONDOMU.



NUSU ya watu wanaotumia kondomu kwa
ajili ya kujikinga na mimba ama magonjwa
ya zinaa, hawajui namna ya kuitumia mipira
hiyo, utafiti umeeleza.

Utafiti huo mpya ulifanywa na Taasisi Moja hivi
ya Kinsley inayohusika
na Utafiti wa Masuala ya Jinsia, Jinsi na
Uzalishaji katika Chuo Kikuu cha Indiana.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa
katika nchi 14 ikiwamo Tanzania katika
kipindi cha miaka 16 iliyopita kuanzia
mwaka 1995 hadi 2011, watu wengi
wamekuwa wakifanya makosa kwa namna
mbalimbali katika kutumia kandomu
ikiwamo uvaaji.

“Makosa yanayofanywa mara kwa mara na
watumiaji wa kondomu ni pamoja na
kuingiza kinga hiyo nusu katika uume
wakati wa ngono au kuitoa kabla tendo hilo
halijamalizika au kusubiri mpaka isinyae,”
Imesema sehemu ya utafiti huo.
Makosa mengine ni kutoacha nafasi katika
ncha ya kondomu kwa ajili ya mbegu za
kiume na kuzifungua vibaya katika pakiti
yake.

Jambo hilo linalosababisha kucha kuzitoboa
na hatimaye kupitisha mbegu au majimaji
kwenda kwa mwanamke,” umeeleza utafiti
huo.

Utafiti huo umeonyesha kuwa makosa
mengine ni kuigeuza kondomu ndani-nje,
kuihifadhi katika sehemu isiyostahili na
kurudia kuitumia katika tendo lingine la
ngono.

Kuivua vibaya: Asilimia 57 ya watu
waliohojiwa, walikiri kuvua kondomu
kimakosa baada ya tendo la ngono. Kati yao
asilimia 27 walikuwa wanawake na asilimia
31 ni wanaume.

Pamoja na makosa hayo ya uvaaji wa
kondomu, watafiti nchini India
wanatarajiwa kufanya utafiti mwingine
mkubwa kuhusu suala hilo kubaini sababu
yake.

Watafiti hao waliamua kufanya uchunguzi
baada ya kubainika kuwapo kwa wanaume
ambao maumbile yao ni makubwa au
madogo kuliko mipira hiyo ya kiume.
Hata hivyo, kondomu zinazopatikana nchini
Tanzania hazitofautiani ukubwa.

Makosa yanayofanywa
wakati wa kutumia mipira hiyo
yanachochewa na watumiaji wenyewe na
kukosekana kwa msisitizo wa elimu ya
namna ya kuzitumia kondomu hizo kutoka
kwa watengenezaji au taasisi za Ukimwi.

Makundi tofauti yalijumuishwa katika utafiti
huo wakiwemo wanandoa,
wafanyabiashara ya ngono na wanafunzi
wa vyuo.
Kati ya asilimia 17 na 51.1 ya watu
walioulizwa maswali katika utafiti huo
walikiri kuwa huingiza kondomu nusu
katika uume wakati wa tendo la ngono.

“Kuvaa kondomu nusu
uume hakuzuii maambukizi kwa sababu
majimaji huwepo wakati wote wakati wa
kitendo hicho na si wakati mwanamume au
mwanamke anapomwaga mbegu zake tu.”

Matokeo mengine yalionyesha kuwa kati ya
asilimia 1.5 na 24.8 ya watu waliowahi
kufanya mapenzi kwa kutumia mipira
walikiri kuchelewa kuvua mipira hiyo wakati
wa tendo.

Aidha, ulibainisha kuwa zaidi ya asilimia
25.3 walikosea kuvaa kondomu kwa
kuikunjua kabla ya kuiivaa badala ya
kufanya hivyo inapoingizwa katika uume.
Zaidi ya nusu ya watumiaji hao walikiri
kuwa walishindwa kuacha nafasi katika
ncha au chuchu ya kondomu ambapo
mbegu hutakiwa kukaa.

Kati ya asilimia nane na 40.7 walisema
wamewahi kukumbana na mkasa wa
kondomu kupasuka katikati ya tendo hilo.
“Utafiti wa kina zaidi unahitajika kufanyika
katika nchi zinazoendelea kwa sababu huku
tunagundua tatizo la kutumia mara mbili
kondomu hasa kutokana na umaskini na
elimu duni,”

Utafiti huu ulisema matangazo mengi ya
kondomu yanajikita katika kueleza ubora
wa kinga hiyo na kusahau kuonyesha
matumizi sahihi na salama.

Kauli toka  Tacaids Tume ya Kudhibiti
Ukimwi (Tacaids),
Wamekiri
tatizo hilo na akaeleza kuwa kama jitihada
za makusudi hazitafanyika kubadili tabia za
watu, hili ni janga kwa nchi zinazoendelea.
Watanzania
wengi hawajui matumizi sahihi ya mipira
hiyo na kuna uzembe katika kulishughulikia
suala hilo katika ngazi ya kitaifa.
“Hiyo ni kweli kabisa. Wengi hawajui
kutumia mipira ya kiume na ni jambo
muhimu watu waelimishwe, uzembe ni wa
hali ya juu sana,” Tacaids wanasema.


Kazi ya Tacaids ni kufanya tathmini
ya kondomu zinavyosambazwa maeneo
mbalimbali nchini na kudhibiti kiasi
kinachotakiwa. Haijihusishi na kufuatilia
namna zinavyotumika.
“Kutumia kondomu ni muhimu, lakini
matumizi salama ni muhimu zaidi hasa
katika nchi zinazoendelea,”

Wasemavyo watumiaji
Mkazi mmoja wa Dodoma,
 alisema anayafahamu baadhi ya
mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa
kuvaa mipira ya kiume, lakini alisahau
kuzingatia wakati wa kuvua.


Mwingine nae, ambaye yeye hutumia
kondomu kama njia ya uzazi wa mpango
alikiri kuwa kondomu iliwahi kupasuka
wakati wa tendo la ndoa.

Mwanafunzi wa kike toka chuo Fulani Nchini,
alisema yeye havai kondomu, huhakikisha
kuwa anamvalisha mwenza wake kabla ya
tendo, lakini huwa hazingatii kanuni za
matumizi salama ya mipira hiyo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linathibitisha
kuwa kondomu inaweza kuzuia mimba na
magonjwa ya zinaa kwa asilimia 98,
imebainishwa kuwa watumiaji wengi wa
mipira hiyo hawaitumii ipasavyo jambo
linalosababisha maambukizi ya virusi vya
Ukimwi, mimba na magonjwa mengine ya
zinaa.

Hebu tuzingatie matumizi sahihi ya kondomu
Ili tuwezekufikia Lengo Halisi
La matumizi ya Kondomu.

0 comments:

Post a Comment