Thursday, 12 September 2013

KAMA HUJUI KUFA TAZAMA KABURI

 

Mtoto huyu asiye na hatia amefikwa na mauti kwa sababu ya jeuri na kiburi cha watu wachache ambao wanadhani wao wana haki zaidi kuliko binadamu wengine kiasi cha kuamua kumwaga damu kadri wapendavyo
Mateso anayopata mtoto huyu ni matokeo mengine ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu na kuiingiza nchi katika baa la njaa na magonjwa ya utapiamlo. Walioanzisha vita hivi hawakujali kwamba watakao athirika ni pamoja na wake zao na watoto wao wadogo wasiokuwa na hatia.
Watoto hawa wachanga (nchini Syria) wamefikwa na mauti kabla hata hawajaijua dunia. Vifo vyao vimesababishwa na watu wenye roho mbaya, choyo, uchu wa madaraka na kutothamini maisha ya watu wengine.
Vita havina macho. Wanaotamani kuanisha vita huwa hawakumbuki au hawajali kwamba moto wanaouwasha ukishasambaa utawarudia na kuwateketeza na wao pia.
 Mojawapo ya njia rahisi ya kujifunza (kuelimika) ni kuiga kutoka kwa watu wengine wenye akili, uwezo na upeo wa hali ya juu kuliko wewe. Hata hivyo ni vema na BUSARA kuiga mambo MEMA, yenye faida na MANUFAA katika maisha yako. Mtu anaekurupuka kuiga mambo ya kipumbavu, yenye madhara, na yanayomtia katika janga la kuweza kuhatarisha maisha yake mwenyewe bila shaka ana WALAKINI. Naam, hiyo ni busara ya kawaida na haihitaji mtu kuwa neural surgeon au space engineer kuliona hili.
 TAFAKARI

0 comments:

Post a Comment