Saturday, 7 September 2013

MAISHA NI SAFARI;HIZI NDIZO KAZI WALIZOKUA WAKIZIFANYA MASTAA HAWA KABLA YA KUWA MAARUFU


Whoopi Goldberg alikuwa anafanya kazi mortuary kusafisha watu waliokufa.

Kanye West alikuwa afisa masoko msaidizi wa Gap.


Mariah Carey alikwishawahi kufanya kazi Saluni, alikuwa akifanya kazi za pembeni kama vile kufagia nywele, kupanga vitu na baadae kutengeneza nywele watu.

B.o.B alikuwa mtengeneza sandwich za Subway.

Nicki Minaji alikwishawahi kuwa Secretary, na pia aliwahi kufanya kazi katika msaada.

Flo Rida, huyu alikuwa akifanya kazi Casino huko Las Vegas, na alikuwa amepigika kiasi cha kuwa anakagua sehemu za kutupa takataka kuona kama kuna chochote cha thamani ambacho mteja anaweza kuwa alitupa.

P. Diddy, huyu aliwahi kufanya kazi El Torito, restaurant moja huko Mexico, na alikuwa akisafisha maeneo ya chooni.

Rick Ross, kama ambavyo wengi wamekuwa wakifahamu, aliwahi kuwa Askari Magereza, na baada ya kukana kuwahi kufanya kazi hii kwa muda, hatimaye mtu mzima alilifikiria hili kwa busara na kukiri kuwa ni kweli aliwahi ku-hustle kwa kazi hii.
Madonna; kabla ya umaarufu alikuwa anafanya kazi ya kuuza Donuts pamoja na Kahawa ambapo alifukuzwa kazi hiyo kutokana na utendaji mbovu.
Credit to Kengete Blog

0 comments:

Post a Comment